Sunday, 23 March 2008
zantel yajikita zanzibar
KAMPUNI ya Simu za Mkononi ya Zanzitel ya Zanzibar, itatiliana saini mkataba wa mwaka mmoja na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) kwa ajili ya udhamini wa Ligi Kuu Zanzibar.
Msemaji wa ZFA, Hamad Maulid Hamad alisema jana kuwa Zantel itatoa Sh 109 milioni kwa udhamini wa ligi hiyo ityakayokuwa ikifanyika kwenye Viwanja vya Amaan, Unguja na Gombani, Pemba. Ligi hiyo ilianza Machi Mosi.
Hamad, alisema kuwa baada ya kukamilishiana udhamini na utilianaji saini, timu zote 12 za Ligi Kuu zitakabidhiwa vifaa mbalimbali ikiwemo jezi, viatu na vifaa vingine.
Alisema kuwa baada ya makabidhiano hayo yatakayoshuhudiwa na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi, Shamsi Vuai Nahodha, kutakuwa na mechi rasmi ya uzinduzi wa ligi hiyo kati ya mabingwa watetezi, Miembeni na Malindi kwenye Uwanja wa Amaan.
Kufunguka kwa milango ya udhamini wa ligi hiyo ya Zanzuibar, kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuinua kiwango cha soka katika visiwa vya Zanzibar hali iliyofanya ligi hiyo kudorora na hata kufanya vibaya kwa timu za visiwani mwaka huu katika mechi za kimataifa.
Mara kadhaa, Kampuni ya Bia Tanzania, TBL kupitia bia yake ya Safari, ilikubali kudhamini ligi hiyo, lakini hata hivyo udhamini wake ulikataliwa kutokana na kile kilichoelezwa kupigwa marufuku kwa matangazo na udhamini wa pombe.
Tanzania Bara ilianza siku nyingi kudhaminiwa ligi yake, ilianza na Safari Lager kabla ya mkataba kuvunjika na sasa Ligi hiyo inadhaminiwa na Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom.
source na gazeti la mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment