Sunday, 23 March 2008

Miembeni ijifunze ilipotoka

Miembeni ijifunze ilipotoka


Tangu kuchukua nafasi ya Ukurugenzi wa wa timu ya Miembeni, Amani Makungu amekuwa ni moja ya wadau wanaopaza sauti zao katika vyombo vya habari, ni kiongozi anaeonyesha kwamba ni mzungumzaji na pia ni mfadhili mzuri anaetoa ofa kadhaa kwa washabiki ya soka visiwani humo kwenda kuona mechi bure. Miembeni ni mojawapo ya timu kongwe visiwani, ambayo imewahi kuwa na mafanikio makubwa kisoka miaka ya nyuma ambapo matajiri kadhaa walijikita katika timu hiyo na kabla ya kudorora na kupotea katika ramani ya soka hasa kipindi cha miaka ya tisini. Ni wazi ni timu hiyo kwa sasa imeshikwa shikwa na vigogo kadhaa ya siasa na hata watu wenye heshima Serekelaini
Ni timu ambayo kwa sasa ndio iliubeba utajiri wa kifedha kuliko timu yoyote ile visiwani.

Timu hiyo ambayo ipo kwenye kitongoji cha Miembeni karibu kabisa na majumba ya maendeleo michenzani , ilitwaa ubingwa wa visiwa hivyo mara ya mwisho yapata miaka ishirini(1987) kwa kutumia Njia ya mahakama baada ya kulazwa na Small samba 2-1 katika uwanja wa amani baada ya Small Simba kumchezesha Shaban Mussa mechi ambayo iliisha kwa ngumi kati ya wachezaji wa timu hizo mbili . Lakini hivi karibuni tu imerejesha heshima yake kwa kulibeba tena kombe hilo ikiwa na Billionea wa kizenj A. Makungu na kocha Suleiman Mahmoud Jabri ambae tayari amejiunga na malindi kutokana na kukosana na mkurugezi huyo
Ufadhili wa Mkurugenzi huyu umewawezesha wapenda soka na washabiki wengi wa timu hiyo kuweza kuona mechi kubwa ya klabu hiyo bila ya viingilio. Mechi yakaribuni ya bure ni ile ya ligi ya Zanzibar kati ya Malindi na Miembeni ambapo Miembeni ilishinda 1-0 lakini pia hatusahau mechi ya kombe la mapinduzi ambapo Miembeni iliweza kutwaa kombe hilo baada ya kuifunga timu ya Polisi kwa mabao 2-1. Mechi hiyo ya dezo ilihidhuriwa pia na Mh. Aman Karume Rais Zanzibar.

Lakini kweli ufadhili huu uliota mizizi kwa miembeni ndio chanzo cha miembeni kupata maendeleo makubwa na kuanza kupata mwanga wa nyota kurudi enzi zake za zamani ?au tu ndio chambo cha kifo chake chengine baada ya kupata pumzi kwa sasa?

Japo tunaomaini ufadhili huu unasaidia Miembeni kujikwamua kisoka, lakini hakuna budi kutasau kidonda kilichowakumba miamba ya soka visiwani hapa baada ya kukimbiwa na wafadhili wakubwa ambao walizipandisha timu zao hadi kileleni na kuziacha zikiwa na mafanikio huku wakiamini timu hizo haziarudi juu.

Baada ya wadhafili wakubwa kujitoa kugharamia timu kubwa huko visiwani, soka la visiwani lilianguka sana, kuanzia katika mechi za ndani hadi za kimataifa. Ukiangalia nyuma kidogo kama miaka kumi iliyopita hasa katika kipindi cha miaka ya 1996-1998, kulikuwa na upinzani mkubwa wa vilabu kutokana na utajili wa wafadhili wao. Timu ambazo zilikuwa zikivuma kipindi hicho ni Mlandege, Malindi na Shangani, ambazo zote zilikuwa chini ya ufadhili wa wafanyabiashara. Timu kama ya Malindi iliweza hata kuzibomoa Yanga na Simba au hata kusajili wachezaji toka Ulaya ya Mashariki na Afrika vilevile. Huku timu kama Kikwajuni na Small Simba ambazo hazikuwa na wafadhili ziliporomoka vibaya katika kiwango cha soka visiwani humo.
Baada ya wafanyabiashara hao kuipa mgongo timu hzio , timu za za serekali ziakaanza kushika kasi na kutesa visiwani hapa. Timu kama KMKM ambayo ilikuwa tishio katika miaka ya 80 ikarudi tena, huku timu ya Polisi ,Jku ,kipanga na Mafunzo, zikaibuka visiwani hapa na kuwa wawakilishi wa wazanzibar katika michezo ya kitaifa na kimataifa kuchukua ubingwa wa Zanzibar na kujiwekea historia zao.
Miembeni inawapasa kutofumba macho katika suala la kuona timu hiyo inabaki kung'ara kama zamani. Ni wajibu wa kila mwanachama, mpenzi na shabiki wa klabu hiyo kukuna kichwa ni kwa namna gani anaweza kuchangia kuona timu hiyo inakuwa na maendeleo endelevu, badala ya kuendelea kumtazama mtu mmoja akifanya kila kitu kwa klabu hiyo kongwe visiwani. Matokea ya ufadhili wa mtu mfanyabiashara yapo wazi kwa kablu kadhaa za visiwani humo baada ya kushika kasi huanguka kama tereni ilioksea njia. Hivyo ni vema kujifunza kutokana makosa waliofanya badala ya kungojea lawama na matukio mabaya ya baadae.
Lakini na mfadhili ajue kwamba anahaki ya kupanga mikakati ya kuiendeleza timu hiyo kwa kuwaachia vitega uchumi vingi ili kuinua timu hiyo badala ya pesa za reja reja na kaucha kutumia timu kama mgongo wa kipato chake.
Kwani ajue jamii na wanamichezo wanamungalia yeye na wanajifunza walipoanguka kutokana ufadhili wa Matajiri wa malindi na mlandege badala ya kusherekea unynyu wa viingilio bure

Juma Said
Mwandihi wa michezo Zanzibar
0713 881046
www.jumaznz.blogspot.com

No comments: