Saturday, 29 March 2008

Robin Lopez has game -- enough game to woo Michelle Wie


Stanford's Robin Lopez is officially the most interesting guy in the NCAA tournament. I don't care if I learn tomorrow that Drew Lavender is actually the bastard lovechild of Ben Vereen and Condoleeza Rice, I still think Robin Lopez has him beat.

Not only do he and his brother -- his identical 7-foot twin -- have an obsession with Disney World, and not only are they both huge Michael Jackson fans, but Robin's also dating Michelle Wie.

mwameja

Mkapa, Mohammed Hussein walichemsha Simba tulipoilamba Yanga 4-1 mwaka 1994


MOHAMED MWAMEJA:

“Tulipoingia kipindi cha pili tuliendelea kuwashambulia Yanga na nakumbuka katika dakika ya 76 hivi, Simba tulifanya shambulizi moja kali langoni mwa timu ya Yanga na kufanikiwa kupata bao la tatu. Bao letu hilo lilifungwa na Madaraka Selemani

TIMU ya Simba ya Dar es Salaam kwa miaka mingi iliyopita imebahatika kuwa na makipa mahiri ambao waliweza kutamba ndani na hata nje ya nchi.

Katika miaka ya 1990, mmoja wa makipa ambaye klabu hiyo ya Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam ilibahatika kumpata si mwingine, bali ni Mohamed Mwameja.

Mwameja kabla ya kujiunga na Simba alivuma sana akiwa na timu za Ndovu ya Arusha na Coastal Union ya Tanga.

Kutokana na umahiri wake mkubwa katika namba yake hiyo, haikuchukua muda mrefu akiwa na klabu ya Simba alichaguliwa kujiunga na timu ya Taifa (Taifa Stars).

Kutokana na uwezo aliokuwa nao wa kulinda lango lake vizuri, wapenzi wa soka walimbatiza jina la Tanzania One, ikiwa na maana kuwa ndiye kipa namba moja wa Tanzania au timu ya Taifa.

Sifa aliyokuwa nayo nyingine ni udakaji wa mipira ya penalti ambayo ilimpatia sifa kubwa hapa nchini pamoja na Afrika Mashariki na Kati.

Hivi karibuni gazeti la DIMBA lilifanya mahojiano naye kuhusu mechi anayoikumbuka vizuri wakati wa enzi zake za kucheza soka ya ushindani.

Katika mahojiano hayo anasema pamoja na kucheza mechi nyingi wakati anacheza soka ya ushindani, lakini kuna mechi moja ambayo anaikumbuka vizuri mpaka leo hii.

Mechi hiyo ni wakati alipokuwa na timu yake ya Simba walipocheza na wapinzani wao wa jadi, Yanga. Anasema mechi hiyo ilikuwa ni ngumu na yenye upinzani mkali, kwa sababu kila timu ilikuwa inataka kuibuka mshindi.

"Simba tuliipania sana mechi hiyo kwa sababu mechi ya mwisho tulipocheza na Yanga walitufunga mabao 2-0 katika mzunguko wa kwanza.

“Nakumbuka mechi hiyo ilichezwa siku ya Jumamosi, Julai 2, mwaka 1994 katika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na ilikuwa ni mashindano ya ligi daraja la kwanza Tanzania Bara (sasa Ligi Kuu) na matokeo yalikuwa ni mazuri kwetu Simba, kwani tuliwafunga Yanga mabao 4-1.

“Mchezo ulianza taratibu, huku kila timu ikiusoma mchezo wa mwenzake. Pamoja na kuanza taratibu lakini ni sisi Simba ambao tulikuwa tunapeleka mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga.

“Nakumbuka katika dakika ya 10 hivi, Simba tulifanya shambulizi moja la nguvu langoni mwa timu ya Yanga na kufanikiwa kupata bao lililofungwa na Athumani China, lakini mwamuzi Bakari Mtangi alilikataa bao hilo na kusema kuwa China alikuwa ameotea.

“Baada ya kushambulia kwa kipindi kirefu kidogo katika dakika ya 16 hivi hatimaye Simba tulifanikiwa kupata bao la kuongoza lililofungwa na George Masatu kwa mpira wa adhabu.

“Bao hilo lilipatikana baada ya Nico Bambaga kumfanyia madhambi mshambuliaji wetu Edward Chumila.

“Haukupita muda mrefu Yanga nao walifanya shambulizi moja la nguvu langoni kwetu na kufanikiwa kusawazisha. Bao lao lilifungwa na mlinzi wao aliyecheza vizuri siku hiyo, Costantino Kimanda kwa mpira wa adhabu ndogo.

“Baada ya Simba kufungwa bao hilo, tuliendelea kuwashambulia Yanga na katika dakika ya 34 hivi ya kipindi hicho cha kwanza tulifanikiwa kupata bao la pili.

“Bao hilo lilifungwa na Athumani China kwa mpira wa kona iliyopigwa na George Masatu.

“Nakumbuka katika kipindi hicho cha kwanza Yanga walimpumzisha Kenneth Mkapa na nafasi yake kuchukuliwa na Willy Martin. Pia walimtoa Mohamed Hussein ‘Mmachinga’ na nafasi yake kuchukuliwa na Ally Yusuf ‘Tigana’.

“Mpaka tunakwenda mapumziko Simba tulikuwa mbele kwa mabao 2-1.

“Tulipoingia kipindi cha pili tuliendelea kuwashambulia Yanga na nakumbuka katika dakika ya 76 hivi, Simba tulifanya shambulizi moja kali langoni mwa timu ya Yanga na kufanikiwa kupata bao la tatu. Bao letu hilo lilifungwa na Madaraka Selemani.

“Pia nakumbuka katika kipindi hicho cha pili mwamuzi wa mchezo huo, Bakari Mtangi alimtoa nje ya uwanja mlinzi Willy Martin wa Yanga kwa kumpiga kichwa cha nyuma mshambuliaji wetu Dua Said.

“Baada ya kuwafunga Yanga mabao matatu tuliendelea kuwashambulia Yanga na walionekana kuzidiwa kabisa na mashambulizi yaliyokuwa yakifanywa na washambuliaji wetu.

“Nakumbuka katika dakika za mwisho mwisho wakati tukiendelea kuwashambulia, tulifanikiwa kupata bao la nne baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa timu ya Yanga.

“Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika Simba tulitoka uwanjani tukiwa wababe kwa kuwafunga Yanga mabao 4-1.

“Ninaikumbuka mechi hiyo kwa sababu mbili, kwanza ilikuwa ni mechi ngumu na yenye ushindani mkubwa sana. Wachezaji wa Simba kabla ya kucheza mechi hiyo tulikuwa na ‘tension’ kubwa na kudhani kuwa hatuwezi kuwafunga Yanga.

“Pili ninaikumbuka mechi hiyo kwa sababu mechi ya mwisho kucheza na Yanga Simba tulifungwa mabao 2-0, hivyo na sisi tulilipa kisasi kwa kuwafunga mabao 4-1.

“Nakumbuka kikosi chetu Simba kilichocheza na Yanga kilikuwa ni mimi, Godwin Aswile, Deo Mkuki, Mustapha Hoza, George Masatu, Iddi Seleman, Athumani China, Hussein Masha/George Lucas, Madaraka Seleman, Edward Chumila (sasa marehemu) na Dua Said.

“Kikosi cha Yanga kilichocheza siku hiyo kilikuwa, Stephen Nemes, Seleman Mkati, Kenneth Mkapa/Willy Martin, Salum Kabunda, Costantino Kimanda, Nico Bambaga, Mohamed Hussein/Ally Yusuf ‘Tigana’, Sekilojo Chambua, Said Mwamba ‘Kizota’ (sasa marehemu), James Tungaraza na Edibily Lunyamila.

“Hiyo ndiyo mechi ninayoikumbuka vizuri sana mpaka leo hii na ambayo siwezi kuisahau maishani mwangu.”

Maelezo haya yamechukuliwa na Henry Paul mjini Dar es Salaam.

Wasifu Wake:
Jina: Mohamed Mwameja
Umri: Miaka 44
Mchezo: Soka
Nafasi: Golikipa
Timu: Makidile (Tanga), Bandari (Tanga), Ndovu (Arusha), Coastal Union na
Taifa Stars.
Kazi: Biashara.

man and arsenal


backam atisha England




hata mkinuna, beckam bado yupo juu england

Tuanzie kwa Fabregas, Mascherano na Ronaldo


Tuanzie kwa Fabregas, Mascherano na Ronaldo



MIAKA michache iliyopita, Cristiano Ronaldo angeweza kuingia uwanjani akiwa mchezaji nadhifu, mwenye sura nzuri na zaidi ya yote, mwenye kipaji kuliko wachezaji wote uwanjani.

Hili la kipaji lilitazamwa zaidi. Angeweza kupiga chenga zake kwa madaha zaidi, akawakimbiza mabeki kwa kadri alivyoweza, akapiga kanzu, tobo na manjonjo mengine kwa madaha, lakini mwishowe asingepiga pasi ya mwisho au kufunga bao.

Katika sehemu nyingi ambazo mashabiki wa soka wanapenda kutazama mipira jijini Dar es Salaam, walipendelea kumuita Ronaldo kazi bure. Huyu hakuwa mchezaji mahiri japokuwa alikuwa na kipaji kikubwa.

Kwa sasa dunia inamshuhudia Ronaldo aliye mahiri. Si kwamba amebadilika sana kiuchezaji, hapana, Ronaldo ni yule yule, isipokuwa maamuzi yake ya mwisho yanamfanya awe na rekodi bora uwanjani. Ama atafunga au kutoa pasi ya mwisho.

Kuna vitu vingi vinavyomfanya mwanasoka awe mahiri. Mashabiki wengi wa Tanzania tunawaangalia wanasoka wetu kijuujuu.

Mwanasoka mahiri ni yule mwenye matokeo uwanjani bila kujali kama ana kipaji kikubwa au hapana. Haijalishi kama una uwezo wa kupiga chenga uwanja mzima, kama huwezi kuisaidia timu kupata matokeo mazuri, huwezi kuwa mchezaji mahiri.

Mpaka wakati naandika makala hii, kwa mujibu wa takwimu za uwanjani, Ronaldo alikuwa mchezaji aliyepiga mashuti mengi zaidi katika lango la adui katika Ligi Kuu ya England. Alikuwa amepiga mashuti 90 yaliyolenga lango la adui.

Utaongeza nini kutoka kwake zaidi ya mabao yake 21 ya ligi yanayomfanya awe mchezaji wa nafasi ya kiungo wa pembeni aliyefunga mabao mengi zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England.

Amewaziba midomo mashabiki wengi wa soka ambao walikuwa wanamzomea katika viwanja vya soka na sehemu za kutazamia mechi za Ligi Kuu ya England.

Miaka kadhaa nyuma, Edibily Jonas Lunyamila alifanikiwa kuwa mmoja wa wachezaji wa aina hii. Achilia mbali uwezo wake wa kusisimua jukwaa, lakini alicheza mpira wa matokeo zaidi kuliko viungo wa pembeni wa sasa.

Halafu mtazame vizuri Cesc Fabregas. Huyu ni kiungo ambaye mashabiki wengi wa soka wanajikuta wakimtukuza bila ya kuchunguza ni kitu gani kinampa umaarufu.

Hana uwezo wa kupiga chenga maridadi na hata umbo lake mwenyewe halimruhusu. Si mpiga kanzu wala tobo, lakini ana uwezo mkubwa wa kupiga pasi za mwisho, achilia mbali kufunga.

Kwa mujibu wa takwimu za uwanjani za Ligi Kuu ya England, Fabregas ndiye mchezaji pekee katika Ligi Kuu ya England anayeongoza kwa kupiga pasi nyingi zaidi. Kabla ya mechi ya leo dhidi ya Wigan Athletic, tayari amepiga pasi 1,676.

Kwa upande wa pasi za mwisho ambazo zilizaa mabao, amepiga 12, huku akiwa amezidiwa pasi mbili na kiungo wa pembeni wa Aston Villa, Ashley Young ambaye amepiga pasi 14.

Ukienda Uwanja wa Taifa utakutana na viungo wetu wengi ambao wengi tunawapa ‘vichwa’ kwa ajili ya mambo ya kipuuzi uwanjani, tobo, kanzu, na visigino ambavyo havizai mabao wala ‘move’ ya maana.

Kwa anachofanya kwa sasa nimeweza kukiona kwa wachezaji wachache sana katika miaka ya karibuni. Haruna Moshi na John Barasa ni miongoni mwa wachezaji ambao miaka ya karibuni waliweza kutuonyesha namna ya kupiga pasi za mwisho.

Lakini pia unaweza kumtazama mchezaji kama Javier Mascherano wa Liverpool. Huyu ni aina ya wachezaji wa kutazamwa uwanjani, kwa sababu katika soka la kisasa mashabiki wanajikita zaidi katika kushabikia wachezaji ambao ni rahisi kuyaona matokeo ya kazi zao.

Mara nyingi viungo wa ulinzi hawahesabiwi kama wachezaji hodari uwanjani na hata wakati wa usajili unapowadia, washambuliaji na viungo wanatazamwa kwa jicho la husuda zaidi.

Katika timu wachezaji wa aina yake ni muhimu mno. Unachoweza kujifunza kutoka kwa Mascherano ni uwezo wa kujitolea uwanjani kwa asilimia 100.

Ili uwe mchezaji kamili unapaswa ucheze kwa ajili ya timu. Ushinde kwa ajili ya timu, na moyo wako uwe umelazwa uwanjani kwa ajili ya timu.

Mpaka naandika makala hii, Mascherano alikuwa mchezaji aliyepora mipira mara nyingi zaidi katika ligi kuu ya England. Alikuwa amepora mipira mara 129.

Huwezi kupora mipira mingi uwanjani kwa bahati, unatakiwa kupigana na hasa katika Ligi Kuu ya England ambayo nayo washambuliaji na wachezaji wa nafasi ya kiungo ni wababe kama wachezaji wetu wa enzi za zamani.

Wakati umepita sasa kusifia wachezaji kihisia hisia. Kuna wachezaji wanapigiwa debe kila kukicha waitwe katika timu ya Taifa. Na wapo mashabiki wanaomtukana kocha wa timu ya taifa, Marcio Maximo pindi anapowaacha wachezaji fulani fulani.

Nadhani wakati umefika walau tuanze kutunza kumbukumbu zetu pindi tunapomshawishi kocha amchague au kumpanga mchezaji fulani katika timu ya taifa au klabuni.

Unapojaribu kumshawishi kocha amuite mchezaji fulani katika timu ya taifa, unaweza kujikumbusha kwamba amepiga pasi ngapi za mwisho na rekodi nyingine ndogo ndogo.

Bahati mbaya hata aina ya ushangiliaji wetu bado ni wa kizamani. Inawakilisha hisia zetu zinazowaelekeza wachezaji wetu wasifanye mambo ya maana uwanjani. Mchezaji anapiga chenga maridadi huku akielekea katika lango lake mwenyewe, inatusaidia nini?

Mchezaji anazunguka katikati ya uwanja na baadaye anatoa pasi ya kisigino kwa Nadir Cannavaro, jukwaa lake linalipuka kwa shangwe kubwa, inatusaidia nini?

Ukiutazama mchezo wa soka kwa sasa, kuna wachezaji wengi wenye vipaji vikubwa lakini hawana msaada mkubwa katika timu. Na sasa makocha mbalimbali barani Ulaya wanajaribu kuepuka wachezaji wa namna hii.

Mchezaji kama Denilson wa Brazil alipewa kipaji kikubwa cha kumiliki mpira. Hata hivyo hakuwa na faida ya ushindi uwanjani na badala yake makocha wa Brazil wakamtumia kama mchezaji wa kupoteza muda uwanjani pindi timu inapokuwa inaongoza.

Na wapo makocha ambao wamekuwa wakiwachezesha wachezaji wengi ambao hawana vipaji vya soka, lakini wanaongoza kwa kutimiza majukumu yao uwanjani.

Tukianza kulitambua tatizo hili, wachezaji wengi chipukizi watajilea katika mazingira ya kuisaidia timu kwa njia mbalimbali na si kufurahisha majukwaa kama inavyotokea kwa wachezaji wengi wa zama hizi.

Lakini kwanza tuwaonyeshe rekodi hizi za akina Ronaldo, Mascherano na Fabregas. Tukizielewa na wenyewe wakazielewa, tutapata kizazi cha wanasoka wenye malengo uwanjani

Torres amewaziba midomo Waingereza


Torres amewaziba midomo Waingereza


HAKUNA neno rahisi wanalopachikwa wachezaji wengi mahiri walionunuliwa kwa bei mbaya katika Ligi Kuu ya England kisha wakashindwa kuonyesha makali yao kama neno Flop.

Hili ni neno la kejeli linalomaanisha kushindwa kwa hali ya juu. Ni neno la dharau na chungu miongoni mwa wachezaji wengi wa kigeni wanaotua England na kushindwa kuonyesha makali yao.

Kamuulize mshambuliaji wa Ukraine, Andriy Shevchenko ni neno gani la Kiingereza alilolielewa kwa wepesi mkubwa atakwambia ni neno Flop.

Sababu kubwa ni ukweli kwamba hili ni neno ambalo kila kukicha limekuwa likitumika kama kejeli kwake na magazeti mbalimbali ya Uingereza kama vile The Sun, The Independent, The Guardian na mengineyo.

Kisa ni wivu mkubwa miongoni mwa mashabiki na vyombo vya Habari vya Uingereza pindi mchezaji mahiri kutoka taifa jingine anapotua Uingereza kwa sifa nyingi na kununuliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha.


Kwa wasiowajua Waingereza, kwao ni halali kwa mchezaji wa Kiingereza kununuliwa fedha nyingi, lakini si kwa mchezaji wa nje.

Na ndiyo maana mpaka leo wako kimya na hawataki kuzungumzia ‘upotevu’ wa fedha uliofanywa na Tottenham Hotspurs kumsajili mshambuliaji Darren Bent kwa kiasi cha Pauni milioni 17.

Ndiyo maana mpaka leo wako kimya kuuzungumzia usajili wa Francis Jeffers, ambaye Arsene Wenger alimsajili kwa makeke kutoka Everton kwa uhamisho uliovunja rekodi ya Arsenal wakati huo, Pauni milioni 10, akaishia kucheza mechi 22 tu na kufunga mabao manne.

Wako wachezaji wengi wa aina hii, lakini kwa sababu ni Waingereza, neno la Flop huwa halitumiwi sana. Zinazungumzwa lugha nyingine za kuficha ukali wa dharau.

Lakini kwa Shevchenko kila siku ni kelele. Na si kwa Shevchenko tu, kina Juan Sebastian Veron, Hernan Crespo, Jose Antonio Reyes, Michael Ballack na wengineo wengi walikumbana na neno flop kwa umaarufu mkubwa kuliko wachezaji wengine wa Kiingereza.

Alipowasili Fernando Torres, huku akivunja rekodi ya uhamisho wa klabu kubwa kama Liverpool, kwa kusajili kwa kiasi cha Pauni milioni 21, zaidi ya Sh bilioni 46 za Tanzania, mashabiki wengi wa Kiingereza walikaa mkao wa kula kushuhudia namna ambavyo mshambuliaji huyu angeshindwa kuonyesha makali yake.

Lakini utasema nini kuhusu Torres? Kabla hata Ligi Kuu ya England haijaisha, tayari ameshawaziba midomo mashabiki ambao walikaa mkao wa kula kuukejeli usajili wake kwa kumuita Flop.

Katika mechi 35 alizoichezea Liverpool hadi wakati naandika makala hii, tayari alikuwa ameshafunga mabao 26 katika michuano ambayo Liverpool inashiriki.

Kikubwa zaidi ni katika Ligi Kuu ya England. Tangu kuondoka kwa Michael Owen mwaka 2004, hakukuwepo na mshambuliaji wa Liverpool aliyefanikiwa kufikisha mabao 20 ya ligi kwa msimu mmoja.

Wamepita na wamekuja wengi kabla yake wakiwemo kina Djibril Cisse, Peter Crouch, Dirk Kuyt na wengineo, lakini hawakuweza kufikisha mabao 20 ya ligi kwa msimu.

Kwa Torres, akiwa sambamba na Emmanuel Adebayor wa Arsenal, tayari ana mabao 19. na zikiwa zimebaki mechi tisa kwa timu yake kumaliza ligi, ni nani anayeweza kucheza kamari na kusema Torres hatafunga bao la 20 na zaidi?

Baada ya kuondoka kwa Owen pia, hakukuwepo na mshambuliaji yeyote wa Liverpool ambaye aliweza kufunga mabao 10 mpaka kufikia kipindi cha sikuu ya Krismasi.

Lakini hilo limekuwa jambo dogo kwa Torres. Waingereza wanatakia nini zaidi?

Siku kadhaa zilizopita alifunga mabao matatu matatu (hat trick) katika mechi mbili mfululizo ndani ya uwanja wa Anfield.


Kwanza ilikuwa Februari 23 alipofunga mabao matatu dhidi ya Middlesbrough, halafu akafunga mabao matatu tena katika mechi dhidi ya West Ham Machi 5.

Kwa kufanya hivi, alikuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Liverpool tangu mwaka 1946 kufunga hat trick mbili mfululizo katika uwanja wa Anfield.

Kabla ya hapo ni mchezaji Jackie Balmer aliyefanya hivyo miaka 62 iliyopita. Waingereza wanataka nini zaidi?

Zaidi ya yote amewapa mashabiki wa Liverpool mdomo wa kusemea ambao mwanzoni hawakuwa nao. Imekuwa lugha rahisi kwa mashabiki wa Manchester United, Arsenal na Chelsea kutambia wachezaji wao.

Kelele za mashabiki wa timu hizi hata wale waliopo Tanzania zilikuwa zinawazungumzia kina Didier Drogba, Thierry Henry, Ruud van Nistelrooy na sasa hivi Emmanuel Adebayor na Cristiano Ronaldo

Liverpool hawakuwa na mdomo wa kusemea kwa sababu mfungaji wao bora alikuwa anatoka katika sehemu ya kiungo, Steven Gerrard. Lakini sasa hawashikiki mitaani kwa sababu wanaye mshambuliaji wa kujivunia, Torres.

Hata hivyo ukiwa mbali Tanzania ni rahisi kudhani kila Muingereza anakenua meno kutokana na mafanikio ya Torres, lakini ukweli hauko hivyo.

Mafanikio ya Torres yanawaumiza kwa upande mmoja. Kwa kiasi fulani yanaendeleza mkondo ule ule wa Ligi Kuu ya England kutawaliwa na wageni kutoka nje.

Kama ungetaka kujua ni kwa namna gani mafanikio hayo yanawaumiza Waingereza, basi ni pale ambapo Torres angeshindwa kung’ara katika msimu wake wa kwanza na kisha akamaliza ligi akiwa amefunga mabao sita tu ya msimu.

Angekejeliwa kwa kila namna na hasa kile kiasi cha fedha ambacho kilitumika kumsajili.

Zaidi ya yote ni ukweli kwamba mashabiki wengi wa Kiingereza walipenda kuona kocha Rafael Benitez wa Liverpool akimrudisha nyumbani kipenzi chao, Owen.

Si kwamba nawachukia Waingereza, hapana, wana wachezaji mahiri. Tatizo kubwa ni namna ambavyo kelele zao za vyombo vya habari zilivyowapandisha wachezaji wao bei kubwa kuliko hali halisi.

Chelsea ilimsajili ‘Muingereza’ Chris Sutton akitokea Blackburn Rovers kwa ada kubwa ya uhamisho wakati huo Pauni milioni 10. Hata hivyo Sutton alifunga bao moja katika mechi 28.

Msimu uliofuata aliuzwa kimya kimya kwenda Celtic kwa uhamisho wa Pauni milioni 6. Hata hivyo hatukusikia kelele nyingi kama ambavyo zimesikika kutokana na kuchemsha kwa Shevchenko.

Anapotokea mchezaji wa aina ya Torres mara nyingi kelele hizi huwa hatuzisikii. Mpaka pale anaposhindwa ndio tunasikia kelele nyingi za kuwakejeli.

Binafsi namtazama Torres kwa jicho tofauti kidogo. Namtazama kwa jicho la kuwaziba midomo mashabiki na vyombo vya habari vya Uingereza ambavyo vinamwaga kejeli kubwa kwa wachezaji wa kigeni waliosajiliwa kwa fedha nyingi pindi wanaposhindwa kuonyesha makali yao.

Wanafanya hivi wakati wachezaji wao wenyewe wa ndani wananunuliwa kwa bei kubwa, lakini wanashindwa kuonyesha makali yoyote ambayo yanaweza kulinganishwa na bei zao kama Torres alivyofanya.

Anachofanya Torres kwa sasa ni kujitafutia usingizi mtamu kwa siku za usoni.

Walau ameweza kupunguza kelele nyingi dirishani kwake ambazo zingekuja kama angefunga mabao sita tu ya msimu kwa uhamisho wake wa Pauni milioni 21.

Mhimili wa Arsenal uliotumika kuteketeza wazee wa AC Milan



Mhimili wa Arsenal uliotumika kuteketeza wazee wa AC Milan


ARSENAL kwa sasa imekuwa timu ya kwanza ya England kushinda kwenye Uwanja wa San Siro, baada ya kuibwaga AC Milan ya Italia kwa mabao 2-0, katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya Jumanne iliyopita.



Alikuwa ni kiungo chipukizi mwenye umri wa miaka 20, Francesc Fabregas Soler au Cesc Fabregas kama alivyozoeleka mbele ya mashabiki, ambaye alikuwa wa kwanza kufungua ukurasa wa mabao kwa shuti la umbali wa mita 30.


Ama hakika mechi hiyo ilidhihirisha kupevuka kwa vijana au ‘Watoto wa Kocha Arsene Wenger’ na jambo la kufurahisha zaidi ni namna ambavyo Fabregas alicheza soka ya kiwango cha juu katika mechi hiyo ambayo imeifanya Arsenal kufuzu hatua ya Robo Fainali, baada ya sare ya bila kufungana katika mechi ya kwanza ambayo Arsenal ilikuwa mwenyeji.

Jambo jingine lililowafurahisha mashabiki wa Arsenal katika mechi hiyo ni namna Fabregas alivyocheza soka ya kuvutia kiasi cha kuwafunika wakongwe wa Milan, katika mechi ambayo ilitafsiriwa na wengi kuwa ni vita ya vijana na wazee wazoefu, akiwamo Paolo Maldini, anayeelekea umri wa miaka 40.

Wengi waliangalia namna wazoefu hao walivyochoshwa na watoto wa Wenger, hususan katika safu ya kiungo, ambako mwanasoka bora wa dunia, Ricardo Kaka alikuwa na wakati mgumu mbele ya Fabregas, ambaye kwa hakika katika mechi hiyo alimfunika, kwani ndiye aliyekuwa mchezaji nyota.

Ushindi huo umeacha swali moja kubwa, nalo ni je, Arsenal baada ya kuwabwaga mabingwa watetezi wa taji hilo, mabingwa ambao wana rekodi ya kulibeba taji hilo mara saba, wataweza kulibeba hapo Mei 21 katika mechi ya fainali huko Moscow, Urusi?


Hakuwa Fabregas pekee katika kundi hilo la watoto wa Wenger aliyefanya maajabu, bali nyota mwingine aliyewakuna wengi alikuwa ni chipukizi wa miaka 18, Theo Walcott, ambaye pasi yake murua ilitosha kuipa Arsenal bao la pili.

Walcott ambaye hivi karibuni alishutumiwa namna kasi ya kukua kwa soka yake ilivyo chini, alidhihirisha kwamba yuko makini, baada ya kuambaa na mpira na kupiga krosi safi ya chinichini iliyomkuta Emmanuel Adebayor, ambaye aliujaza mpira wavuni kiulaini.

Wakati mashabiki wakiendelea kusubiri mambo mazuri ya Walcott kadri siku zinavyozidi kwenda, gumzo kubwa kwa sasa ni kuhusu Fabregas, ambaye ni wazi amekuwa lulu na kiongozi wa chipukizi wenzake katika kuhakikisha wakongwe wa AC Milan wanaziaga fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya kwenye uwanja wao wa nyumbani.

Fabregas, aliyezaliwa Mei 4, 1987, Arenys de Mar, Hispania, ni mchezaji aliyeibukia katika klabu ya Barcelona akiwa kijana mdogo na hapana shaka klabu hiyo huenda inajuta kwa kumuacha aondoke, kwani kwa sasa ni lulu katika klabu ya Arsenal.

Wakati huo anakumbukwa zaidi namna alivyokuwa mahiri katika safu ya kiungo, lakini zaidi alikuwa ni kiungo mkabaji, ingawa mara kadhaa pia alionyesha umahiri katika kuzifumania nyavu kwa mabao yake safi na ya kuvutia na wakati mwingine alifunga mabao hata 30 kwa msimu mmoja.

Hofu ya kutopata nafasi ya kuitwa katika kikosi cha kwanza ilimuingia na hapo akaanza mipango ya kuihama Barcelona na ndipo alipotua rasmi Arsenal, Septemba 2003.

Siku zake za mwanzo zilikuwa ngumu katika jiji la London, hata hivyo urafiki wa karibu na mchezaji mwenzake, Philippe Senderos ulikuwa na msaada mkubwa kwa Fabregas, ambaye alizoea maisha na hata kuyafurahia.

Akiwa kijana wa miaka 16, Fabregas hakuwa na mawazo ya kupata nafasi katika kikosi cha kwanza mapema, alikuwa ni mwenye kuwaangalia wakongwe, Gilberto Silva na Patrick Vieira, wakati huo huo alikuwa makini katika mazoezi, huku akijifunza lugha ya Kiingereza.

Alicheza mechi yake ya kwanza mwezi mmoja baada ya kujiunga na timu hiyo, mechi ambayo ilikuwa ni ya Kombe la Ligi dhidi ya Rotherham United na hivyo kujiwekea rekodi ya kuwa mchezaji chipukizi mwenye umri mdogo kupata namba katika kikosi cha kwanza cha Arsenal.


Katika mechi iliyofuata ambayo pia ilikuwa ni ya Kombe la Ligi, akiwa na miaka 16 na siku 177, Fabregas alikuwa chipukizi wa kwanza mwenye umri mdogo kufunga bao katika klabu ya Arsenal, ambayo katika mechi hiyo ilitoka na ushindi wa mabao 5–1 dhidi ya Wolves. Arsenal ilitwaa taji la Ligi Kuu msimu wa 2003/04, huku ikiwa na rekodi nzuri ya kutofungwa hata mechi moja, lakini Fabregas hakupewa medali ya ushindi huo kwa sababu hakucheza mechi hata moja ya ligi hiyo.

Mechi nyingine ya ushindani na ambayo inaweza kutajwa kuwa ya kujivunia katika siku za mwanzo mwanzo za Fabregas katika klabu ya Arsenal, ni ile ya kufungua msimu, mechi ya kuwania Ngao ya Jamii dhidi ya Manchester United, iliyochezwa mwanzoni mwa msimu wa 2004/05.

Hadi hapo tayari jina lake lilianza kuwa gumzo na aliwafurahisha wengi alipofunga bao wakati Arsenal ikiibugiza Blackburn mabao 3-0 katika mechi ya Ligi Kuu ya England na baada ya hapo aliendelea kuwa na namba, hususan alipoumia Vieira.

Balaa la majeruhi lilipoendelea kuiandama Arsenal kwa kuwakumba wachezaji wake, kina Edu na Gilberto Silva, Fabregas aliendelea kupata nafasi katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, hususan alipocheza Arsenal ilipoumana na Rosenborg na kuibuka na ushindi wa mabao 5–1 na yeye kufunga bao moja.

Fabregas aling’ara kwa mara nyingine na kujipatia taji lake la kwanza katika Kombe la FA, akiwa katika kikosi cha kwanza alitoa mchango mkubwa kwa timu yake ambayo ilitwaa taji hilo kwa kuing’oa Man United kwa mikwaju ya penalti, hiyo ilikuwa ni mwaka 2005.

Kuondoka kwa Vieira ambaye alijiunga na Juventus ya Italia ilikuwa ni kufungua ukurasa mpya kwa Fabregas, ambaye alirithi jezi namba nne ya Vieira na akawa anashirikiana vyema na Gilberto katika safu ya kiungo, alicheza jumla ya mechi 49 katika msimu wa 2005/06 na licha ya kuwa na umri mdogo lakini kiwango chake cha uchezaji kilikuwa kivutio.

Wako waliohofia uwezo wake katika kumrithi Vieira, lakini mwenyewe baada ya kuaminiwa na Wenger alikuwa na staili yake ya kipekee ya kiuchezaji na wachambuzi wengi wa soka walifurahishwa na namna alivyocheza vizuri katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Juventus na Real Madrid.

Katika Ligi ya Mabingwa Ulaya aliiwezesha timu hiyo kufikia hatua ya fainali na kumana na klabu yake ya zamani ya Barcelona, mechi iliyochezwa Mei 2006, lakini ilishindwa kufurukuta mbele ya Barcelona ambayo hatimaye ililibeba taji hilo, huku Arsenal ikimaliza msimu wa 2005/06 bila kombe.

Baada ya msimu huo, uvumi wa Fabregas kuihama Arsenal ulianza kuibuka, hususan Real Madrid ilielezea wazi wazi nia yake ya kutaka kumsajili kiungo huyo, lakini mwenyewe aliuzima uvumi huo Oktoba 2006, baada ya kusaini mkataba mpya wa miaka sita na timu hiyo huku akidai kwamba anavutiwa na staili ya uchezaji ya Arsenal pamoja na imani kwa kocha wake Wenger.

Msimu wa 2006/07 ulikuwa ni wa mafanikio binafsi kwa Fabregas ambaye aliendelea kuwa nuru, alipata tuzo ya Golden Boy ya gazeti la michezo la Tutto Sport la Italia, alipata tuzo ya mwanasoka bora wa mwezi Januari 2007 wa Ligi Kuu ya England, pia alikuwamo katika timu bora ya mwaka 2006 ya UEFA pamoja na tuzo ya mwanasoka bora wa msimu wa Arsenal.

Kinachowafurahisha mashabiki wengi wa Arsenal kwa Fabregas si tuzo anazopata, bali ni aina yake ya uchezaji ambayo bila shaka ndiyo iliyomwezesha kupata umaarufu alionao sasa na hata kuwa gumzo duniani.

Ni kiungo ambaye wakati wote amekuwa muhimu na mwenye mchango katika kikosi cha kwanza cha Arsenal na pengine kilichotokea katika mechi na AC Milan ni sehemu tu ya mambo mazuri ambayo amekuwa akiyafanya.

Anaiongoza timu vizuri kuanzia safu ya kiungo, ni mbunifu mwenye mbinu za uhakika, anawapa wenzake pasi nzuri na wakati wote si mbinafsi anapokuwa na mpira, ni mahiri katika kupiga kona na jambo la mwisho ni namna anavyodhihirisha ukomavu wa soka lake, jambo ambalo kutokana na umri wake mdogo linaleta matumaini makubwa kwamba mambo mazuri kutoka kwake yataendelea kuonekana.

Kuna wakati aliwahi kulaumiwa na wachezaji wenzake kwa kutumia mbinu na akili zaidi kuliko nguvu, hata kufananishwa na bondia wa uzito mdogo, jambo ambalo ni wazi kwamba kwa sasa amejirekebisha, kwani kadri siku zilivyozidi kwenda amekuwa ni mchezaji wa kutumia nguvu.

Pamoja na umahiri na mafanikio yanayoonekana Arsenal, lakini katika timu ya Taifa ya Hispania, Fabregas bado hajafanya mambo makubwa, alianza kuichezea timu hiyo mwaka 2003 akiwa na timu ya vijana chini ya miaka 17 katika fainali za Kombe la Dunia nchini Finland.

Aliitwa katika timu ya wakubwa kwa mara ya kwanza mapema mwaka 2006 katika mechi ya kirafiki dhidi ya Ivory Coast na baada ya hapo ameendelea kuwa mchezaji muhimu wa timu hiyo na hata kuiwakilisha katika fainali za Kombe la Dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani.

Huyo ndiye Francesc Fabregas Soler, mhimili muhimu wa Arsenal katika harakati za kutwaa taji la Ligi Kuu ya England na lile la Ligi ya Mabingwa Ulaya.

machupa na gabriel hamna wiva


uvumi uliosikika siku za nyuma kwamba washambuliaji wawili mahiri wa Simba, Emmanuel Gabriel na Athuman Machuppa hawaivi vizuri kwa sababu ambazo haziko wazi.

Wakati mwingine hakuna unachoweza kutegemea kutoka kwa washambuliaji wawili wa Kitanzania wanaong’ara pamoja zaidi ya hisia za wivu na hata kurogana

Labda wana hisia kwamba hawawezi kucheza pamoja uwanjani na kila mmoja wao akang’ara. Labda wana hisia kwamba mmoja anamzibia mwenzake nyota yake kung’ara.

Lakini laiti kama ningekuwa mshauri wa Machuppa au Gabriel, kitu kimoja ningewaambia kwa uwazi zaidi kwamba hakuna sababu ya kuoneana wivu wala kurogana.


Kama wote wawili wakizifanya kazi zao kwa ufasaha, kila mmoja anaweza kung’ara uwanjani bila ya kumhofia mwenzie. Na zaidi, kuna uwezekano mkubwa kuwepo kwa wote wawili uwanjani kukawafanya wawe mahiri zaidi pengine kuliko inavyokuwa pale mmoja wao anapokaa nje ya uwanja.

Kwa nini? Kwa sababu hawa ni washambuliaji wawili tofauti ambao kocha yeyote wa soka anaweza kuwatumia uwanjani kutokana na utofauti wa staili zao.

Kwa Gabriel, huyu ni mfungaji asilia ambaye ana uwezo mkubwa wa kuwa kidokozi katika eneo la hatari la adui. Kwa wazungu washambuliaji wa aina hii huwa wanaitwa fox in the box au goal getter

Na hata mchambuzi wa soka, mlinzi mahiri wa zamani wa Manchester United, Paul Parker alipata hisia hizo wakati alipokuwa akichambua mechi kati ya Simba na Prisons iliyoonyeshwa moja kwa moja na kituo cha Televisheni cha kulipia cha GTV ambako Gabriel alifunga mabao matatu (hat trick)

Ukimtazama Gabriel ni wazi kwamba hana ubora mwingi akiwa mbali na eneo la hatari. Hana kasi wala uwezo mkubwa wa kutambuka walinzi na kwenda zake kupachika bao.

Ubora wake mkubwa uko katika kupachika mabao akiwa karibu na eneo la hatari. Na huu si ujinga bali ni kipaji cha hali ya juu kwa sababu si kila mchezaji ana uwezo mkubwa wa kujiweka katika maeneo ya hatari na kufunga.

Baada ya ushuhuda wa kuondoka kwa Zamoyoni Mogella ‘original’ wa miaka ya 1980, halafu akaja Mohamed Hussein wa miaka 1990 na kisha akaondoka zake, walau unaweza kusema Gabriel ndiye ‘shetani’ wa eneo la hatari aliyefuatia katika miaka ya 2000

Mchezo wa wachezaji wa aina hii unahitaji msaada mkubwa kutoka kwa wachezaji wa nafasi za viungo wa ushambuliaji, mshambuliaji anayecheza nyuma yake (playmaker) au pia mawinga wa pembeni.

Ukitazama namna Gabriel alivyoikimbilia nafasi yake katika pambano la Ashanti wakati akisubiri krosi ya Ramadhan Wasso, ni wazi mtazamaji angejua kwamba kilichofuata kingekuwa bao.

Wakati Wasso akikimbizana na mpira katika upande wa kushoto, Gabriel alikuwa bize akijitafutia nafasi ya karibu kabisa na lango huku walinzi wa Ashanti na baadhi ya washambuliaji wa Simba wakitegea.

Krosi ilipompita kipa wa Ashanti ilitua katika kichwa chake. Hakuhitaji kuupiga kichwa mpira ule zaidi ya kuegesha tu mpira ugonge kichwa.

Huyu ndiye Gabriel, lakini jaribu kumtazama Machuppa. Ana staili tofauti ya uchezaji na ana tofauti kubwa na Gabriel.

Machuppa ana uwezo mkubwa wa kushambulia akiwa mbali na lango. Kasi yake ya mchezo ni kubwa na hasa wakati ule alipokuwa mchezaji chipukizi. Bahati nzuri, ana ‘jicho’ zuri afikapo langoni mwa adui.

Unaweza kutumia neno ‘bahati’ kwa sababu ni washambuliaji wachache wenye kasi na uwezo wa kutambuka mabeki ambao wana shabaha nzuri ya kufunga.

Washambuliaji wengi wenye kasi za marathon au uwezo wa kuwatoka walinzi, hawana shabaha kubwa katika ufungaji kuliko wale ambao Mwenyezi Mungu amewapa kipawa cha kuvizia kama Gabriel.

Ukichunguza kwa mifano ya Ulaya, japo wachezaji wetu hawajaweza walau kunusa ubora wa kufananishwa na wachezaji wa Ulaya, unaweza kuifananisha hali hii kwa kuwatazama washambuliaji Thierry Henry wa Barcelona na Ruud Van Nisterlooy wa Manchester United.

Hawa tunawafahamu kwa sababu tuliwatazama kwa kipindi kirefu katika ile ligi iliyozoeleka zaidi Tanzania yaani Ligi Kuu ya England.

Henry pamoja na kasi yake na ubora wake mwingi, lakini ni wazi kwamba hakuwa na shabaha kali ya lango kama ilivyo kwa Van Nisterlooy. Kinyume chake ni hivyo hivyo, Van Nisterlooy pamoja na shabaha yake kali langoni, lakini hakuwa msumbufu kwa walinzi

Je watu wa aina hii hawawezi kucheza pamoja? Je Machuppa na Gabriel hawawezi kucheza pamoja? Jibu ni hapana. Watu hawa wanaweza kucheza tena kwa ufanisi mkubwa.

Katika mifumo ya kisasa mmoja anaweza kucheza mbele na mwingine akacheza nyuma yake. Na kwa kuwatazama wote wawili, Machuppa, kutokana na kuwa na kasi kubwa, ana uwezo wa kurudi mpaka katikati ya uwanja na kuchukua mipira kwa watu wa nafasi ya kiungo.

Kwa kasi yake anapaswa kuwa na visheni kubwa ya kupiga pasi za mwisho kwa sababu ana uwezo mkubwa wa kuwatoka walinzi na kutengeneza nafasi kwa wengine.

Kufunga ni majaliwa, lakini kitu kikubwa ni kwamba unapokuwa na uwezo wa aina hii, unapata fursa kubwa ya kutengeneza mabao kwa wengine. Na ndio maana ulitokea msimu ambao Henry alifanikiwa kupiga pasi za mwisho 24 na kuvunja rekodi za pasi za mwisho zilizozaa mabao katika Ligi Kuu ya England.

Kwa Gabriel anaweza kunufaika na kasi ya Machuppa kwa kufungua nafasi za kufunga kwa sababu kuna ukweli kwamba walinzi wanahangaika zaidi na mchezaji aliye na mpira na mwenye kasi kuliko ambaye amejificha nyuma ya kivuli akifungua nafasi.

Bahati mbaya kuna walinzi ambao siku zote wanahaingaika na mchezaji anayefungua zaidi nafasi kuliko mwenye mpira. Hali hii iliwakuta walinzi wa Arsenal katika mechi ya Nusu Fainali ya Kombe la FA uwanja wa Villa Park mwaka 1999.

Walinzi wa timu hiyo walijishughulisha zaidi na wachezaji wa Manchester United waliokuwa wamefungua nafasi, kuliko Ryan Giggs aliyekuwa na mpira. Waliposhtuka Giggs alikuwa anaingia katika eneo lao la hatari na hatimaye kumtungua kipa David Seaman.

Kwa mtindo kama huu, Machuppa na Gabriel wanaweza kutumiana kwa njia moja au nyingine katika kupasiana au kufunguliana nafasi. Na bahati nzuri, kila mmoja ni bora katika aina tofauti ya mchezo anayotumia.

Hii lugha ya ‘kurogana’ ingeweza kuvuma au kueleweka kama wachezaji hawa wangekuwa Mohamed Hussein na Gabriel. Wote hawa ni wachezaji wa aina moja na walau wangeweza kuzibiana bahati.

Ni wazi kwamba kama Gabriel na Machuppa hawapendani au ‘wanarogana’ kama tunavyoelezwa basi ni kwa sababu ya kuogopa vivuli vyao au kutojiamini katika uwezo wa vipaji vyao tofauti.

Kama kila mmoja akiifanya kazi yake kwa ufasaha ni wazi kwamba wana uwezo wa kucheza pamoja na kuwa mahiri kwa pamoja. Tatizo ni lile lile la wachezaji wetu kutojiamini na kufikiria kwamba Simba na Yanga wamefika.

Na hata ukimlazimisha Gabriel acheze mpira wa Machupa hawezi kufanya hivyo, na ukimlazimisha Machupa acheze katika staili ya Gabriel utakuwa unalazimisha vitu visivyowezekana. Ni kulazimisha vitu visivyowezekana.

Thursday, 27 March 2008



Ali Saleh akiwa picha ya pamoja na vijana huku Farouk karrim akiwa ameva afulana ni wadau wakubwa wa michezo visiwani
licha ya kuwa watangazaji wa bbc na redio one, lakini wanasukuma gurudumu la maendeleo ya michezo

Zantel kweli imekusudia au inajaribu tu?


eti kweli Zantel atasaidia timu zetu au timu ndio zitasaidia Zantel?

Timu za pemba zaanza kutisha

Timu za Pemba zaanaza kutisha
Jku jana ililala kwa mabao 3-0 dhidi ya chipukizi katika uwnaj wa amani
jUZI Miembeni walitoka 1-1 na Jamhuri ya Pemba

zanzibar tuwe kama Arsenal



Arsenal walimu wazuri



ILIKUWA Machi 4, 2008 wakati vijana wadogo kiumri na wanaoonekana kutokuwa wazoefu wa mikiki mikiki mikubwa ya soka la mashindano makubwa, Arsenal kutoka London walipofanya jambo ambalo halikutarajiwa na wengi.

Vijana hao waliivua ubingwa wa Ulaya timu kubwa na maarufu duniani ya AC Milan ya Italia iliyojaa wachezaji maarufu sana, wenye uzoefu sana na waliowahi kupata mafanikio makubwa sana ya soka Ulaya na duniani kwa ujumla.




ADEBAYOR na Fabregas wakishangilia goli

Cha kusisimua ni kwamba vijana hao wa London walifanya jambo hilo kubwa kwa mabao 2-0 ya Cesc Fabregas na Emmanuel Adebayor walioupata kwenye uwanja wa San Siro wa wakali hao wa Italia.

Kabla ya siku hiyo hakuna timu yoyote ya Uingereza iliyoweza kuishinda timu hiyo ya Italia kwenye uwanja huo.

Ukiitazama kwa makini mipango ya timu ya Arsenal na ushindi walioupata dhidi ya AC Milan ugenini baada ya kutoka suluhu katika mechi ya awali iliyopigwa kwenye Uwanja wao wa Emirates jijini London wiki mbili zilizotangulia, utapata mafunzo yafuatayo:-

Mpira wa miguu ni mchezo wa vijana wadogo Ukiiangalia orodha ya wachezaji wa Arsenal "waliouangusha mbuyu" San Siro, utabaini kwamba wastani wa umri wao ni miaka kama 22 hivi ambapo wastani wa umri wa wachezaji wa AC Milan unakaribia miaka 30.

Wastani wa umri wa wachezaji wa Arsenal ungekuwa mdogo zaidi wasingekuwapo kina kipa Almunia, nahodha Gallas na Gilberto Silva aliyeingia dakika za mwisho.

Kwa upande mwingine, wastani wa umri wa wachezaji wa AC Milan ungekuwa mkubwa zaidi kama wasingecheza kina Pato na Kaka.

Katika hali hiyo, ni wazi wachezaji wa Arsenal walikuwa na pumzi zaidi kuliko wa AC Milan. Isingekuwa ajabu kwao kushinda hata kwa mabao 3-0 kwenye dakika za nyongeza kama AC Milan wangebana hadi pambano kufika dakika 90 likiwa suluhu.

Ni wazi wakati huo AC Milan wangekuwa wamekwisha kabisa kipumzi. Kwa hiyo funzo la kwanza tunalolipata kutoka kwa Arsenal ni kwamba soka ni mchezo wa mafanikio kwa timu yenye vijana wadogo wengi.

La msingi ni kuwa na vijana wadogo wenye vipaji na kuwapa maandalizi mazuri.

Tuwaamini wachezaji wa soka wenye umri mdogo.

Funzo la pili tunalojifunza kutoka kwa Arsenal ni kuwaamini wachezaji wadogo. Kwa kufanya hivyo, wachezaji hao wanajenga moyo wa kujiamini na wanafanya juhudi kutopoteza imani hiyo waliyopewa.

Mwaka jana, vijana wadogo tupu wa Arsenal ambao sasa ndiyo timu yenyewe ya kikosi cha kwanza waliaminiwa kucheza mashindano ya Kombe la Ligi (Carling Cup) hadi kuifikisha timu fainali.





KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger

Walipofika fainali, walikumbana na timu kubwa na ngumu ya Chelsea. Wengi waliamini kocha wao Arsene Wenger angebadili kikosi hicho lakini alichezesha hicho hicho cha vijana wadogo bila kujali kukosa taji ambalo msimu huo lingekuwa pekee. Walifungwa mabao 2-1 lakini mechi hiyo iliwaongezea kujiamini baada ya kuona wameaminiwa.

Katika kuwaamini wachezaji wake chipukizi, Wenger, hawatelekezi wanapoharibu mechi bali huzidi kuwatumia kuwajengea hali ya kujiamini.

Kwa mfano, miezi ya kati kati ilionekana kijana mdogo sana Theo Walcott alikuwa anashindwa kutoa mchango wa maana kwa timu na baadhi ya watu kushauri kijana huyo auzwe kwa mkopo, jambo ambalo Wenger amelikataa na kuendelea kumuamini.

Matokeo ya kumuamini huko, ni kijana huyo aliyetia krosi iliyopigwa kichwa na Adebayor kilichogonga mwamba kwenye dakika za mwisho za mchezo wa kwanza wa Arsenal na AC Milan.

Aidha, ni kijana huyo mdogo, anayezidiwa miaka 21 na Paolo Maldini wa AC Milan, aliyeruka kwanja kwenye dakika za mwisho kabisa za mechi ya marudiano, kukata mbuga hadi kuingia ndani ya eneo la mita 18 la AC Milan na kutoa pasi kwa Adebayor ya kumuwezesha kufunga kirahisi bao la pili.

Mtoto huyo aliyafanya hayo siku si nyingi baada ya kufunga mabao yote mawili ya Arsenal ilipotoka sare ya 2-2 nyumbani kwa Birmingham City katika Ligi kuu ya England.

Makali yake ya sasa, ambayo ni wazi yataongezeka, ni matokeo ya yeye kuaminiwa kama wanavyoaminiwa wenzake wanaochezea timu hiyo.

Kwenye mashindano, timu zote zina nafasi sawa Kutokana na matokeo ya AC Milan dhidi ya Arsenal tumejifunza pia kwamba timu zinapokuwa mashindanoni kila moja ina nafasi sawa ya kushinda.

Wengi waliokuwa wanaisubiri mechi ya AC Milan na Arsenal hawakutarajia kama Arsenal ingeweza kupata ushindi mkubwa hivyo ugenini lakini Arsenal walishinda.

Timu zetu nazo zijenge utamaduni wa kuamini kuwa zikijipanga vizuri zinaweza kuishinda na kuitupa nje ya mashindano timu yoyote watakayokutana nayo katika mashindano ya vilabu barani Afrika.

Hali ya kujiona wanyonge baada ya kujua watapambana na nani, huzifanya timu zetu zitolewe kabla ya mechi.

Hii si kwa vilabu tu, hata kwa timu ya taifa. Naamini tungekuwa na ujasiri wa Arsenal, mwaka jana Senegal wangeambulia kutoka kwetu, sana sana, pointi moja ya mchezo wa kwao.

Kwa bahati mbaya tulitishwa na jina bila kujua kuwa Senegal hii si ile ya miaka ya nyuma kama ilivyodhihirika kwenye fainali za Ghana. Basi tuwe Arsenal wakati tutakapocheza na Cameroun mwaka huu.

Ushindi hupatikana popote

Jambo la mwisho walilotufundisha Arsenal kwa kuitoa mashindanoni AC Milan ni kwamba ushindi hupatikana popote pale. Hapa kwetu tuna lugha ya ajabu na ya kinyonge. Wawakilishi wetu wanapocheza nyumbani na timu kali kama Al Ahli ya Misri au Esperance ya Tunisia,wanaposhinda kwa bao 1-0, tunasema wamefanya kosa kubwa kwa kushindwa kufunga mabao mengi kama 3-0 au zaidi na hivyo kujiweka katika mazingira magumu kwenye mechi ya marudiano!

Al Ahli ni ndogo kiasi gani mpaka tuipigie hesabu ya mabao 4-0? Hilo 1-0 lenyewe tu, kulipata tunapaswa kushukuru.

Kutokana na kauli hizo, timu yetu inayoshinda hapa kwa ushindi mwembamba, inaenda kwenye mechi ya marudiano ikijihesabu imetolewa tayari! Tujenge utamaduni wa kuamini kuwa ushindi hupatikana popote.

Tunashinda hapa 1-0, tunashinda tena ugenini. Mfano mzuri wa miaka ya karibuni ni wa Yanga. Ilitoka sare ya 2-2 na Highlanders ya Zimbabwe hapa nyumbani lakini ikaenda kushinda 2-0 ugenini kwa mabao ya Ally Yussuf Tigana.

Arsena ni walimu wazuri kwetu. Naomba tulielewe vizuri somo lao kwa mafanikio yetu.

kaka ,ronaldo, messi nani tishio la ulaya?



Kaka, Ronaldo, Messi: Katika kilinge cha ufalme wa kulichezea gozi duniani champion


Tuzo hiyo ambayo hutolewa na Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), itatolewa katika Makao Makuu ya Shirikisho hilo kwenye ukumbi wa Opera House jijini Zurich nchini Uswisi Jumatatu ya Desemba 17 mwaka huu.

Mshindi wa Kombe la Ligi ya mabingwa Ulaya akiwa na AC Milan, Kaka, hana cha kupoteza katika tuzo hiyo kutokana na kuwa na kiwango bora zaidi kwa kipindi cha miezi 12 iliyopita, lakini hicho si kigezo cha kuwabeza washindani wake Ronaldo na Messi.

Ronaldo ametwaa tuzo karibu zote za soka katika ardhi ya nyumbani kwake Ureno na Uingereza anakocheza soka la kulipwa, huku akiifikia rekodi ya mchezaji wa zamani wa Aston Villa na Scotland, Andy Gray aliyoiweka mwaka 1977 ya kutwaa tuzo ya mwansoka bora wa mwaka wa PFA na mchezaji bora chipukizi wa mwaka ndani ya msimu mmoja.

Messi amezidi kuwa na wakati mzuri zaidi katika kikosi chake cha Barcelona na Timu ya Taifa ya Argentina. Ingawa timu yake ilishindwa kutwaa Kombe la Klabu Bingwa Ulaya na la lile la Ligi Kuu ya Hispania msimu uliopita, haitakuwa sababu ya kumzuia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 kutajwa katika tuzo hizo.

Kaka:
Brazil ni sehemu inayozalisha vipaji vingi vya soka duniani. Wengi wakifuata nyao za wachezaji kama Romario, Rivaldo, Ronaldo, Ronaldinho na Ricardo Izecson Santos Leite.

Kaka, anajulikana kwa mashabiki wengi wa soka kutokana na uwezo wake dimbani, kumiliki mpira, kupiga chenga, kutengeza pasi nzuri za kuzaa magoli na maamuzi yake ya haraka anapokuwa na adui, hizo ni baadhi ya sehemu zinazong’arisha kipaji chake.

Historia ya Kaka kuelekea kilele cha mafanikio katika usakataji wa soka ni ya kuvutia. Alikulia katika familia ya maisha ya kati iliyomuwezesha kupata elimu kiurahisi na mahitaji yake yote ya muhimu.
Wakati baba yake Bosco ni Muhandisi kitaaluma, lakini amekuwa akimfuatilia mwanawe na kumsimamia katika kila mkataba ambao anakuwa akiingia kwenye soka.

Akiwa amezaliwa katika mji Mkuu wa Brazil, Brasilia mwaka 1982, Kaka alikulia katika jiji la Sao Paulo baada ya wazazi wake kuhamia huko wakati akiwa na umri wa miaka saba.

Kama ilivyo kwa ndoto za watoto wengi wa umri wake, alipenda kucheza soka kama sehemu ya kujiburudisha kabla ya kuanza kuitilia mkazo alipofikisha umri wa miaka 15.

Hata hivyo, akiwa na umri wa miaka 18, nusura ndoto yake ya kuendelea kucheza soka la kulipwa iyeyuke baada ya kupata ajali iliyomsababisha kuumia mbavu wakati anaogelea kwenye ‘swimming pool’: “Baada ya kupona hakika nilikubali kwamba ni mkono wa Mungu ndiyo ulioniokoa,” ameandika katika kitabu cha maisha yake.

Safari ya Kaka katika maisha ya soka haikuwa na milima na mabonde, kwani ilinyoka. Mwaka 2001, alijikuta yupo katika kikosi cha timu ya vijana cha Sao Paulo. Haraka sana ndani ya umri wake huyo wa miaka 18 tayari ‘alibebwa’ na kuingizwa katika timu ya wakubwa na Januari 31, 2002, aliichezea Timu yake ya Taifa ya Brazil kwa mara ya kwanza dhidi ya Bolivia. Na tangu hapo hakuna kilichomzuia kuelekea kilele cha mafanikio ya usakataji wa soka.

Miaka mitatu baadaye, nyota wa zamani wa timu ya Sao Paulo na AC Milan, Leonardo, ambaye amekuwa akifutilia maendelea ya kipaji cha Kaka kwa karibu zaidi, alimshawishi yeye na familia yake kutafuta timu nchini Italia, kitu alichokubali na kukitekeleza kwa kujiunga na AC Milan wakati wa majira ya joto mwaka 2003.

Katika soka la Ulaya mambo yamezidi kumuendea viuri zaidi, kwani msimu wa mwaka 2003/04 aliisaidia timu yake kutwaa taji la 17 la Ligi Kuu ya Italia, Serie A.

Msimu uliopita alikisaidia kikosi hicho cha Rossoneri kutwaa taji la Ligi ya mabingwa Ulaya, huku yeye akiibuka mfungaji bora wa michuano hiyo akiwa ametikisa nyavu mara 10.

Messi:
Kwa miaka kadhaa saa katika soka la Argentina, mashabiki wamekuwa wakimheshimu kama Diego Maradona.

Mara nyingi amekuwa akikataa na kujiona kwamba bado hajaweza kufikia mafanikio ya Maradona, lakini winga huyo wa Barcelona anayetumia guu la kushoto kutikisa nyavu za goli lolote analolishambulia, alifanya kile alichokifanya El Diego, wakati alipofunga bao dhidi ya timu ya Getafe Aprili mwaka huu.

Alifunga bao la ‘Mkono wa Mungu’ kama alilofunga Maradona akiwa na jezi namba 10 wakati wa mchezo wa robo fainali ya Kombe la Dunia mwaka 1986 dhidi ya Uingereza.

Katika hafla fulani Maradona mwenyewe aliwahi kusema: “Sasa nimemuona mchezaji atakayechukua nafasi yangu katika soka la Argentina na huyo si mwingine bali ni Lionel Messi.”

Akiwa amezaliwa Juni 24 mwaka 1987 jijini Rosario, Santa Fe, Messi amekuwa chachu kubwa ya vijana wengi hivi sasa kujikita katika soka nchini kwake Argentina.

Akiwa na umri wa miaka 13, kutokana na matatizo ya kiuchumu nchini Argentina, aliamua kuhamia Hispania akiwa pamoja na familia yake.

Baada ya kuonyesha kipaji cha hali ya juu wakati akicheza na watoto wenzake katika mitaa ya Barcelona, hatimaye alialikwa katika Dimba la Camp Nou kwa ajili ya majaribio, na kusajiliwa moja kwa moja huku akianza kucheza Ligi ya Hispania kwa mara ya kwanza mwaka 2004.

Bao lake la kwanza alifunga Mei mosi dhidi ya Albacete, na hivyo kuweka historia ya kuwa mchezaji mwenye umri mdogo zaidi kuifungua timu hiyo goli katika Ligi Kuu, ambapo aliivunja rekodi iliyowekwa na Bojan Krkic miaka kadhaa iliyopita.

Mapenzi yake na rangi za blue na nyeupe za Timu ya Taifa ya Argentina yalianza miezi kadhaa baadaye baada ya kuwa stelingi katika Timu ya Taifa ya Vijana chini ya umri wa miaka 20 akiongoza kuifunga Uholazi kwenye Fainali za Kombe la Dunia la U-20 mwaka 2005 ambapo aliibuka na kiatu cha dhahabu baada ya kuwa mfungaji bora.

Agosti mwaka 2004, kocha Jose Nestor Pekerman alimpanga kwa mara ya kwanza Messi kucheza katika kikosi cha Argentina dakika zote 90 kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Hungary.

Ronaldo:
Cristiano Ronaldo Santos Aveiro hakuna shaka kwamba ni moja ya kipaji cha soka kilicho juu zaidi katika ulimwengu wa soka hivi sasa.
Uwezo wake wa kupiga chenga zenye maudhi huku akikimbia kwa kasi ya ajabu akiwa na mpira ni moja ya vitu vilivyowafanya baadhi ya mashabiki kumfananisha na wajina wake Ronaldo Luis Nazario de Lima kutoka Brazil.
Akiwa amezaliwa kwenye Kisiwa cha Madeira Februari tano mwaka 1985 nchini Ureno, alianza safari yake ya soka la kulipwa akiwa na timu ya Nacional kabla ya mwaka 2002 kuhamia kwa miamba ya jiji la Lisbon, Sporting, akiwa na umri wa miaka 17.
Tangua hapo hakuna kilichomzuia kuendeleza kipaji chake katika ulimwengu wa soka la kimataifa. Wakati wa msimu wake huo mmoja akiwa na klabu hiyo alicheza mechi 25 na kufunga mabao matatu.

Wakati mzuri zaidi kwa kipaji cha Cristiano Ronaldo, ni kipindi ambacho Manchester United ilipoomba mechi ya kirafiki dhidi ya Sporting mwaka 2003, wakati ikiwa katika ziara ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Uingereza. Uwezo wake aliouonesha katika mchezo huo ambao Wareno hao walishinda mabao 3-1, kilikuwa kishawishi tosha kwa kocha wa Mashetani Wekundu hao, Sir Alex Ferguson kuamua kumsajili kwa dau kubwa.

Tangu amejiunga na Manchester amekuwa na wakati mzuri wa kufurahia kipaji chake cha soka katika kila sekunde.
Ifuatayo ni orodha ya wanasoka waliowahi kutwaa tuzo ya mwaka soka bora wa dunia, nafasi ya kwanza hadi ya tatu, tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1991, kwenye mabano ni nchi anayotoka mchezaji.

Mwaka 2006
1. Fabio CANNAVARO (Italia)
2. Zinedine ZIDANE (Ufaransa)
3. RONALDINHO (Brazil)

Mwaka 2005
1. RONALDINHO (Brazil)
2. Frank LAMPARD (Uingereza)
3. Samuel ETO’O (Cameroon)

Mwaka 2004
1. RONALDINHO (Brazil)
2. Thierry HENRY (Ufaransa)
3. Andriy SHEVCHENKO (Ukraine)

Mwaka 2003
1. Zinedine ZIDANE (Ufaransa)
2. Thierry HENRY (Ufaransa)
3. RONALDO (Brazil)

Mwaka 2002
1. RONALDO (Brazil)
2. Oliver KAHN (Ujerumani)
3. Zinedine ZIDANE (Ufaransa)

Mwaka 2001
1. LUIS FIGO (Ureno)
2. David BECKHAM (Uingereza)
3. RAUL (Hispania)

Mwaka 2000
1. Zinedine ZIDANE (Ufaransa)
2. LUIS FIGO (Ureno)
3. RIVALDO (Brazil)

Mwaka 1999
1. RIVALDO (Brazil)
2. David BECKHAM (Uingereza)
3. Gabriel BATISTUTA (Argentina)

Mwaka 1998
1. Zinedine ZIDANE (Ufaransa)
2. RONALDO (Brazil)
3. Davor SUKER (Croatia)

Mwaka 1997
1. RONALDO (Brazil)
2. ROBERTO CARLOS (Brazil)
3. Dennis BERGKAMP (Uholanzi)
3. Zinedine ZIDANE (Ufaransa)

Mwaka 1996
1. RONALDO (Brazil)
2. George WEAH (Liberia)
3. Alan SHEARER (Uingereza)

Mwaka 1995
1. George WEAH (Liberia)
2. Paolo MALDINI (Italia)
3. Juergen KLINSMANN (Ujerumani)

Mwaka 1994
1. ROMARIO (Brazil)
2. Hristo STOICHKOV (Bulgaria)
3. Roberto BAGGIO (Italia)

Mwaka 1993
1. Roberto BAGGIO (Italia)
2. ROMARIO (Brazil)
3. Dennis BERGKAMP (Uholanzi)

Mwaka 1992
1. Marco VAN BASTEN (Uholanzi)
2. Hristo STOICHKOV (Bulgaria)
3. Thomas HAESSLER (Ujerumani)

Mwaka 1991
1. Lothar MATTHAEUS (Ujerumani)
2. Jean-Pierre PAPIN (Ufaransa)
3. Gary LINEKER (Uingereza)

maisha ya critiano ronaldo


cristiano :Kinda la Ferguson linalowachungulia Kaka na Ronaldinho Ulaya champion




Klabu ya kwanza kuichezea akiwa kinda ni SL Benfica ambapo baadaye alijiunga na mpinza mkubwa wa timu hiyo, Sporting. Hata hivyo hakudumu kwa muda mrefu, kwani alijiunga na klabu ya Andorinha, ambayo baba yake mzazi alikuwa ni mshirika mkubwa tangu akiwa na umri wa miaka minane.

Mwaka 1995, jina la Ronaldo lilikuwa kubwa nchini Ureno hususan mjini Madeira alipozaliwa, hali hiyo ilisababisha timu mbili za eneo hilo, CS Maritimo na CD Nacional kupigana vikumbo zikitaka kunasa dole gumba lake.

Hata hivyo, timu ya Nacional ndiyo iliyofanikiwa kumnasa mchezaji huyo, lakini baadaye alirejea kuichezea Klabu ya Sporting ambapo alijiunga na kikosi cha Yosso.

Kutokana na uwezo wake kuimarika, alichaguliwa kuichezea Timu ya Taifa ya Ureno katika michuano ya UEFA chini ya umri wa miaka 17 (U-17), kiwango alichokionesha kwenye kitimtim hicho kilimuweka roho juu aliyekuwa Kocha wa Liverpool FC, Gerard Houllier.

Hata hivyo, Houllier alisitisha juhudi za kumnasa kinda huyo kwa madai kwamba umri wake wa miaka 16 aliokuwa nao wakati huo ungemchukua muda mrefu kukomaa kisoka.

Kipigo cha mabao 3-1, Manchester United ilichokipata katika Uwanja wa Lisbon nchini Ureno kutoka kwa Sporting, huku Ronaldo akiwa anawika katika winga ya kulia, kilimtoa Sir Alex Ferguson udenda, ambaye kipindi hicho alikuwa na mikakati ya kutafuta winga Yosso wa kulia.

Majira ya joto, Ferguson alifanikiwa kunasa dole gumba la kinda huyo kwa Pauni za Uingereza milioni 12 ambapo alimpa mikoba ya David Beckham aliyekuwa amehamia Real Madrid ya Hispania.

Ronaldo alikabidhiwa jezi namba saba ambayo inaheshimika Man United, kutokana na kuvaliwa na nyoto muhimu waliowahi kuwika katika klabu hiyo kama George Best, Bryan Robson, Eric Cantona na David Beckham, hiyo ilikuwa kama njozi mpya kwa kinda huyo, kwani awali akiwa Sporting alikuwa akitumia jezi namba 28.

Kama ulivyo mfumo wa Man United kwa washambuliaji wake kucheza kwa kubadilishana namba wawapo uwanjani, Ronaldo amemudu vema utaratibu huo kwani siyo ajabu kumuona akicheza winga ya kulia, mshambuliaji wa kati ama namba kumi.
Oktoba 29, 2005, Ronaldo aliifungia Manchester United goli la 1000 katika Ligi Kuu ya nchini humo maarufu kama ‘Barclays Premiership’, wakati timu hiyo ilipoikandamiza Middlesbrough kwa mabao 4-1.
Desemba 2006, Ronaldo aliwika na kuwa mmoja wa wachezaji muhimu wa Man United, baada ya kuifungia magoli sita katika mechi tatu alizoshuka dimbani.

Julai 8, 2006, wakati Ureno ikicheza na England kwenye robo fainali za kombe la dunia, Wayne Rooney alimtupia lawama Ronaldo kuwa alimshawishi mwamuzi kumtoa nje kwa kadi nyekundu baada ya Rooney kumchezea vibaya, Ricardo
Carvalho.

Kitendo hicho kiliibua mambo mengi kwa wachezaji hao kwani magazeti ya nchini England, The Sun na The Daily Mirror yalichapisha habari kuwa, kutolewa kwa Rooney kuliigharimu timu yao kusukumizwa nje kwenye michuano hiyo kama ilivyokuwa kwa David Beckham mwaka 1998 katika kinyang’anyiro kama hicho.

Suala hilo lilimpandisha mzuka Rooney na kuweka wazi kwamba, Ronaldo atakapokanyaga ardhi ya England kuitumikia Klabu yake ya Man United, atamfanyia kitu mbaya.

Kinda huyo wa Kireno alijibu mapigo kwa kusema kwamba atahamia Real Madrid ya Hispania, hata hivyo Ferguson alimtumia msaidizi wake Carlos Queiroz kuweza kuzungumza na Ronaldo ambapo naye aliweza kuongea na Rooney na hivyo wawili hao wakaelewana.

Suala hilo liliifanya Man United, ilipofika Aprili 13 mwaka 2007, kumsahwishi mchezaji huyo kufunga ndoa ya muda mrefu na klabu hiyo, ambapo alikubali kusaini mkataba mpya utakaomuwezesha kulipwa Pauni 120,000 kwa wiki.

Kitita hicho kinamfanya kuwa wa kwanza kupokea dau kubwa katika historia ya Klabu ya Mashetani Wekundu hao, baada ya kuanguka dole gumba hilo alisema “Ninajisikia furaha kubwa kuwepo katika klabu hii, ninachotaka kwa sasa ni kushinda vikombe zaidi, natumaini hilo litawezekana msimu huu”.
Katika mechi za kimataifa hususan wakati akiichezea timu yake ya taifa Ronaldo aliweza kuifungia Ureno bao la kufutia machozi dhidi ya Ugiriki wakati ilipofungwa mabao 2-1 katika ufunguzi wa michuano ya Mataifa ya Ulaya mwaka 2004.

Kadhalika aliweza kuifungia Ureno bao la kwanza katika nusu fainali hizo dhidi ya Uholanzi, wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa mabao 2-1.

Ronaldo pia aliiwakilisha Ureno katika michuano ya Olimpiki kipindi cha majira ya joto mwaka, 2004, pia alishika nafasi ya pili ya ufungaji bora katika kinyang’anyiro cha kuwania kufuzu kombe la dunia katika ukanda wa Ulaya baada ya kucheka na nyavu mara saba.

Bao lake la kwanza kufunga katika michuano ya kombe la dunia lilikuwa la penaliti dhidi ya Iran.
Februari 6, 2007, yaani ikiwa ni siku moja baada ya kusheherekea siku ya kuzaliwa kwake, Scolari alimtangaza Ronaldo kuwa nahodha wa Ureno katika mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil.

Baada ya kumpa unahodha, Scolari alisema alifanya hivyo kutokana na maagizo aliyopewa na Rais wa Chama cha Soka nchini humo (PFF), Carlos Silva ambaye alifariki dunia siku mbili kabla.

Ronaldo yupo katika mtihani mgumu wa kuwabwaga wachezaji wengine wawili wa Kibrazil Ricardo Izecson dos Santos Leite ‘Kaka’ na Ronaldinho Gaucho ambao wanapewa nafasi kubwa ya kuweza kuibuka mwanasoka bora wa FIFA msimu huu.

Vikombe alivyoshinda akiwa na Manchester United
Ubingwa wa England: 2006-2007
Kombe la FA : 2004
Kombe la Ligi: 2006
Ngao ya jamii: 2007

Jina kamili Cristiano Ronaldo dos Santos Aveiro
Kuzaliwa Februari 5, 1985 (miaka 22)
Alipozaliwa Funchal, Madeira, Ureno
Urefu 1.85 m
Nafasi Mshambuliaji wa pembeni, Kulia
Klabu Manchester United
Jezi namba 7
Timu ya taifa Ureno kuanzia 2003

Makala haya yameandaliwa na ISAAC KIJOTI kwa msaada wa mashirika ya habari ya kimataifa.


Dear Guest you have enter our site without being Registered. We recommend to register to view more...
"Mgeni wetu unatakiwa Kuregista kupata Udaku Wote..."

maximo na makocha wa yanga na simba



Maswali magumu zaidi katika soka ya Tanzania

kwanza. Katika siku za karibuni kumekuwa na rundo la makocha wa kigeni wanaotiririka katika klabu zetu kubwa zenye uwezo wa kuajiri makocha hawa wa bei ghali.

Wanashuka katika uwanja wa ndege pale Kipawa, wanapokewa kwa mbwembwe huku wakionekana kama vile ni malaika. Na ni wazi inaonekana kama vile wanabeba hatima ya klabu zetu ambazo wakati huo zinakuwa hazina makocha.

Ndiyo, na kwa sasa pia kuna rundo la wachezaji wa kigeni ambao wananunuliwa kwa bei ghali. Achana na wachezaji hawa wa kigeni, hata wachezaji wa nyumbani wananunuliwa kwa bei ghali na kila wanapotia saini katika klabu kubwa huwa wanasifiwa kuliko kiasi.

Kwa wageni, wengi wao pamoja na makocha wanalala katika hoteli za kifahari na wanalipwa fedha za kigeni kila mwisho wa mwezi unapowadia. Lakini tunaweza kujiuliza, mbona klabu zetu zimeendelea kukimbizana katika nyumba za wachawi zikijaribu kutafuta uchawi wa ushindi dhidi ya timu nyingine? Kawaulize waganga wa kienyeji watakwambia namna viongozi wa klabu kubwa wanavyopishana kwao kwa ajili ya kusaka ushindi.

Hapa ndipo tunapojiuliza; wachezaji hawa mahiri wa kigeni pamoja na makocha wa Kizungu, wana msaada gani kwa timu kama tuna imani kuwa mganga anaweza kusababisha tutoe kipigo kitakatifu kwa mtani wa jadi au timu pinzani ambayo tunacheza nayo?

Ukizubaa katika swali hili ambalo kamwe haliwezi kukupatia jibu yakinifu, utaumiza moyo wako bure. Kuna hili suala la waamuzi. Wanawindwa kuliko kiasi kwa ajili ya kuzipendelea timu fulani. Majina yao yanatafutwa mapema kabla hata ratiba haijatoka, baadaye wanatafutwa mitaani.

Ina maana gani ya kuleta wachezaji mahiri na kuingia gharama kubwa wakati tuna uwezo wa kumwona mwamuzi? Ina maana gani kumleta kocha wa Kizungu kwa mbwembwe kubwa kama akili yetu ya ushindi ipo kwa mwamuzi na mchawi?

Kwa nini gharama hizo zisitumike kumwongezea dau mganga ili tupate uhakika wa kutwaa ubingwa wa Afrika na makombe mengine ambayo yanakuja mbele yetu? Utaniambia kuwa uchawi hausaidii kama wachezaji hawapo fiti. Tunahitaji majaabu ya kushinda na ndio maana hatuna haja na habari za maslahi ya wachezaji. Inakuwaje mganga anatwambia wachezaji wawe fiti wakati hilo ni jukumu lake kutuwezesha kushinda?

Hatuna uhakika wa ufiti wa wachezaji na ndio maana tumekwenda kwake, iweje tuambiwe kuwa wachezaji wanahitaji kuwa fiti? Swali jingine gumu ni hili la kununua mechi kutoka kwa wachezaji wa timu pinzani. Kama mmenunua waamuzi, mmekwenda kwa waganga, lakini pia mna wachezaji ambao wamewagharimu mamilioni ya fedha pamoja na makocha ambao mmewatoa mbali kwa ajili ya kufundisha mpira, ni kwa nini mkanunue wachezaji wa timu pinzani?

Tena timu pinzani ambayo msimu uliopita tuliinyong’onyesha kwa kwa kusajili wachezaji wake. Ina maana gani ya kuwa na wachezaji wazuri na kocha wa Kizungu kama bado tunanunua wapinzani? Si tungejaribu kuwa na timu ya kawaida na zile gharama za kununua wachezaji na kocha wa kigeni tukazipeleka kwa wachezaji wa timu pinzani ili tushinde mechi zote za ligi? Swali gumu!

Lakini pia tunajiuliza; kwa nini kama mmemalizana na mwamuzi mnalazimika kwenda kumalizana na mchawi? Ina maana hata mwamuzi anapaswa kulindwa na nguvu za kishirikina? Au kwa nini kama mmekwenda kwa mchawi bado mnakwenda tena kuonana na mwamuzi? Ina maana mwamuzi ana nguvu kuliko mchawi ambaye mmempatia Sh milioni 5 chini ya kivuli cha kamati ya ufundi?

Halafu inakuwaje mnaamini katika kila nguvu inayowazunguka? Mnaahidi Sh milioni 5 kwa kila mganga, Sh milioni 5 kwa mwamuzi na Sh milioni 1 kwa kila mchezaji kama mkishinda.

Na zaidi ya yote, mmetoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya wachezaji wa timu pinzani. Katika hao wote mnamwamini nani zaidi?

Ina maana timu ikishinda ni nani atakuwa ameleta ushindi klabuni? Mwamuzi, wachezaji, mchawi au wachezaji wa timu pinzani? Naamini itachukua miaka 100 kumwamini mtu ambaye atajigamba alisababisha timu ishinde.

Na hapo hapo tusisahau kuwa kocha naye atajigamba kuwa amepeleka ushindi klabuni. Atazungumza na vyombo vya habari kuwa wachezaji wamefuata maelekezo yake na ndiyo maana timu imeshinda. Ni nani atambishia?

Bahati mbaya hatuwezi kujibu maswali haya magumu na ndiyo maana tupo hapa tulipo. Kila siku tunamtafuta ‘mchawi’ kwa sababu hatujafahamu kuwa ni sisi wenyewe. Kwa maswali haya magumu ambayo hayawezi kujibika, tunapata taswira halisi ya ubabaishaji uliopo katika soka yetu

Hatuna programu za vijana kwa sababu tunaamini uchawi unaweza kusababisha tushinde mechi. Hatuamini katika soka ya vijana kwa sababu tunaamini kwamba mwamuzi anaweza akapelekea tushinde mechi.

Tunaamini katika soka ya wachezaji wa kigeni kwa sababu tumeshindwa kupata mwendelezo wa wachezaji wenye kaliba ya akina Sunday Manara. Na sasa tunaishi kwa imani zaidi badala ya kufuata misingi halisi ya soka. Kama hatuwezi kujijibu maswali haya magumu tuliyojiuliza, ukweli unabaki pale pale kwamba soka ni mchezo wa sayansi. Hakuna uchawi wala habari ya mwamuzi.

Kama kuna ubishi katika hili basi tuialike Timu ya Taifa ya Brazil tumwone mganga au mwamuzi atakayezuia kipigo dhidi yetu.

Tuondokane na ubabaishaji katika ngazi za chini hadi juu. Hizi si zama za kumwona mwamuzi wala kumtafuta mchawi. Mambo haya tunaweza kuyafanya kwa kujidanganya katika soka yetu ya ndani, lakini katika ngazi za kimataifa tutashindwa.

Waghana walishindwa katika ardhi yao, na kila siku tunaziona timu nyingi ambazo zinashindwa katika ardhi zao. Hata hivyo wenzetu walifanikiwa kujibu maswali haya magumu na ndio maana kila wanaposhindwa wanatafuta mbinu zaidi za kusonga mbele.

Ni lazima tupate swali moja tu; la kwa nini wachezaji wetu hawachezi vizuri uwanjani? Haya ya wachawi, kununua wachezaji wa timu pinzani, kununua waamuzi yamepitwa na wakati na ndiyo ambayo yametubakisha hapa tulipo. Inachekesha sana. Na nadhani ni wakati wa kujibu maswali haya magumu.

Monday, 24 March 2008

miss Zanzibar


januari 13, 1968: miss zanzibar wa kwanza hediye khamis mussa (kati) akipozi na wenzie baada ya kutwaa taji. mashindano hayo yaloandaliwa na chama cha hockey, kama ilivyokuwa kwa bara baada ya shindano la kwanza mwaka 1967, yalipigwa marufuku na hadi hii leo hayajafanyika tena hapa visiwani

black sailor itavuka?

Na Juma Said- Zanzibar



WACHEZAJI WATISHIA KUONGOA UONGOZI BLACK SAILOR



Timu ya black sailor yenye makazi yake mtaa wa kidongo chekundu , inyocheza ligi daraja kwanza visiwani Zanzibar imejikuta ikiwa katika mgogoro kati ya wachezaji pamoja na wanachama wa timu hiyo dhidi ya uongozi waoliopo madarakani.

Mgogoro huo umekuja baada ya timu hiyo kupoteza michezo yake miwili mfululizo dhidi ya kikosi cha zima moto Kwa kufungwa mabao 4 kwa 3 na ile dhidi ya sebleni iliofanika siku ya 18/2/2008 ambapo timu hiyo ilifungwa wa bao 1 na kufanya wachezaji pamoja na wanachama wa timu hiyo kutishia kuongoa uongozi wao madarakani,

Katika hali isiyoyakawaida klabuni hapo wachzaji wa timu hiyo walifanya kikao cha dharura katika dimba la uwanja wa mao baada ya mechi yao dhidi ya sebeleni kilichowafanya wachezaji hao kutoka uwanjani hapo usiku badala wakati wa kawaida, katika kikao hicho klichongozwa na mchezaji mkongwe visiwani hapa ambae aliwahi kuichezea timu a shangani ambacho karibu a viongozi wote`wa juu walikikimbia na kuwahudhuriwa na kiongozi moja tu aliefamika kwa jin la Mohammed Juma kilijadili mambo mengi na moja kati ya`hayo ni kuwataka viongozi hao kujishughulisha zaid na timu au kuwaachia ngazi na timu kuongozwa na wanachama.,

Akitihibitisha habari hizi mjini hapa, mmoja ya wachezaji waaandamizi wa timu alisema kwamba timu hiyo inayomgogoro ambao unafukuta na kama hautatuliwa mapema unaweza kuigawa timu hiyo na kuwa kama timu ya taifa ya Jangombe ambayo hadi hivi sasa imepoteza`sifa yake baada ya kutokea kutolewena,

“Kweli kuna manunguniko ya wazi dhidi ya uongozi na ndio maana kinachotokea sasa kinaonekana cha kupoteza mechi zote hizi,tayari sisi kama wachezaji tumekaa kikao chetu na kutoa mapendekezo yetu” aliendelea kusema” baadhi ya vongozi wapo hapo kwa ajili ya kulinda nafasi zao katika vyama vya soka, lakini hawapo katika kusaidia timu, uongozi umekuwa haujui hasa majukmu yake na kufikia hata kumuingilia kocha katika upangaji wa timu, lakini baya zaidi ni kuigawa timu na kutaka kupangwa wachezaji waliowaleta wao badala kuangalia uwezo wa mtu binafsi” akisema kwa uchungu mchezaji huyo ambae ni miongoni mwa wachezaji walioipandisha kutokea mchangani na pia amekataa kuanikwa jina gazeti , pia alisema uongozi huo umefanya usajili mbaya huku fedha nyingi zikitumika katika usajili huo na kuwatuhumu baadhi ya viongozi kufuja fdha za usajili, alisema baadhi ya wachezaji wamekuwa mzigo kwa timu ambao uwezo wao kisoka umepitwa na wakati lakini wamesajailiwa, pia badhi y wengine wamesajiliwa lakini wameingia mitini kutokana na uongozi kutokuwa makini na usajili.

Huku malalamiko hayo ya wachezaji dhidi ya uongozi yakishika kasi uongozi wa timu hiyo umekanusha kuwepo kwa malalmiko hayo.

Akiongea kwa njia ya simu na mwandishi wa habari hizi,mmoja wa viongozi wa timu hiyo Uled Said Uled alisema sio kweli kwamba timu yao inamgogoro kama huo.

“Sijasikia kufanyika kikao cha wachezaji dhidi ya uongozi, sijasikia kwamba wachezaji pamoja na wanachama wanamatatizo na uongozi , na kwaweli timu yetu ni shwari hadi sasa, mimi ndio nilioushghulikia usajili wote sasa kama hatushguklikii timu ningalifanya hivyo?”, alisema ndugu Uled ambae ni miongoni wa viongozi waliotimuliwa katika timu ya taifa yajangombe na kukimbilia Timu hiyo, alisema kocha wa tim hio yupo huru na hakuna anaemuinglia.

“ mimi huwa sikai katika banch la ufundi, lakini najua hakuna kiongozi mwenye mchzaji wake,wote ni wachzaji wetu kocha yupo huru hupanga kikosi na hao wanaotoa taarifa hizo sio wapenzi wa black sailor” alisema ndugu uled , kuhusu swala la usajili wa timu hiyo kuwa mbovu, alisema kocha ndio aliopendekeza wachezaji , alisema Kigezo cha Mosi Shabani kusajiliwa sio chake bali kocha ndio aliopendekeza kusajiliwa

“Hata huyo Mosi Shabani anaelalamikiwa ameletwa na kocha, lakini pia tangu ianze ligi hajacheza hata mechi moja” alisema ndugu Uledi. Mosi shabani ni mchezaji aliechezea timu za simba ya dare s salaam mnamo miaka ya ya mwanzo mwa thamanini, small simba na malindi na sasa ni miongoni mwa wachezji waliosajiliwa katika usajili wa timu hiyo mbao wadau wengi wa timu hiyo wanautulia shaka uchangiaji wake katika timu hiyo.

Huku hayo yaijiri,habari za kuminika klabuni hapo tayari uongozi wa timu hiyo ulitegemea kufanya kikao cha dharura kujadili hali hiyo na huku baadhi ya viongozi wa timu hiyo wakipanga kuwapa adhabu wachezaji kutokana kuonekana vnainara wa matukio hayo lakini pia baadhi ya viongozi wengine wakipinga aina yoyote ya adhabu ili kuijenga timu. Akithibisha kikao hicho mmoja ya viongozi wa timu hiyo alisema kikao hicho kiltegeme kufanyika 21/2/2008. “kweli tunakikao, lakini ni kikao chetu kitajadili mechi yetu dhidi ya small samba na sio jengine “ alisema kwa ufupi kiongozi huyo

Timu ya black sailor ni miongoni mwa timu zilzopanda daraja mwaka huu.

inayongozwa na rais wa timu hiyo Hamad Maulid Hamad na baadhi ya viongozi waliohamia timu hiyo wakitokea katika timu ya taifa ya Jangombe baada ya kuondolewa madarakani na wanachama kwa tuhuma mbali mbali mnamo mwaka jana

taifa ya jangombe

TAIFA YA JANGOMBE YAJIPANGA UPYA Uongozi wa Timu ya taifa ya jangombe umaarufu Wakombozi wa ng’ambo umesema umenza kujipanga upya kuhaikisha inarudisha heshima yake iliopotea kwa miaka ya hivi karibuni, akizungumza mjini hapa hivi karibuni na gazeti hili kaimu katibu mkuu wa timu hiyo ndugu Nassor Abdallah alisema wameandaa mikakati mikubwa kuhakisha timu hiyo inarudi daraja la kwanza mwakani na pia kuuchukua ubingwa na kuwakilisha Zanzibar katika mechi za kimtaifa kwa mara ya kwanza॥‘ Hii sio ndoto bali ni ukweli uliowazi kwamba tumejipanga , kilichotokea msimu wa ligi uliopita kila mtu anajua kwamba timu ilihujumiwa na ndio maana tukashuka daraja , lakini hatutegemei mara hii kutokea tena kwa swala kama hilo hasa kutokana na sisi viongozi kuwa wamoja na pia kuwaunganisha wanachama ili kuweka nguvu moja ili kurudisha heshima ya timu, tunataka wanachama wetu walijue hilo na wawe wamoja“ Alisema ndugu Abdallah ambae alikua akifuatilia kwa karibu ligi ya vijana inayoendelea jimboni Jangombe Katika kuhakisha timu hiyo inarudi tena daraja la kwanza ndugu Abdallah alisema hivi karibuni wanatarajia kubadili kadi na kutoa kadi mpya kwa wanachama wa timu hiyo na baadae kufanya uchaguzi mkuu wa kuchagua viongozi wa kuendesha timu unaotarajia kufanyika mnamo mwezi wa september mwaka huu ambapo wanachama wanaotakiwa kugombea ni wale tu watakaokuwa na kadi mpya zitazotolewa। Alpoulizwa kawanini wameamua kubadili kadi wakati tayari timu hiyo inazo kadi zinazotambulika ndugu alikataa kuweka wazi “ tuanchoamni kubadili kadi ni moja ya kujenga timu bora itayokuwa na wanachama wenye upendo wa dhat na timu na sio vyenginevyo, lakini kama kunawatu watu wanamaoni tofauti na uongozi basi wanakaribishwa kutoa maoni yao tutayuasikiliza na kuyafanyia kazi yakiwa yanafaa, hatuna nia ya kumzuia mtu asigombee“ alisema ndugu Nassor Lakini Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili limegundua moja ya nia ya kubadili kadi ni kuwazuia viongozi waliondoshwa na wanachama kurudi tena madarakani kwa kuwazuia kugombea nafasi yoyote ya uongozi katika timu hiyo।Kuhus usajili wa wachezaji alisema ni mapema mno kuzungumzia swala hilo lakini nia ya uongozi wake ni kusajili wachezaji kutoka Zanzibar pekee na sio tena Tanzania bara kama ilivuyozoeleka na timu ili kuepusha gharama na pia usumbufu unaotokana na wachezaji hao hasa inapokuwa ligi inapokuwa ipo kati kati।Ili kupata wachezaji watakaounda timu hiyo tayari benchi la ufundi wa timu hiyo unaitupia macho kombe la vijana linaloendelea katika uwanja wa timu hiyo katika mashindano ya kombe la mbuzi ambalo limekuwa kivutio kikubwa jimboni hapo hasa kutokana na kuawshirikisha wachezaji wa timu ya taifa star na ile ya Zanzibar, wachezaji wanaoshiriki ni ABdi kassim (Bab) na wengine wanaocheza daraja la kwanza Zanzibar. Timu ya taifa ya jangombe kati kati ya msimu ilikumbwa na mgogoro mkubwa ambapo baadhi ya viongozi walisimamishwa kuongoza timu hiyo na wanachama.Viongoiz walisimimishwa na aliekuwa rais Hamad maulid hamad, Ndugu Uled katibu msaidizi, Dau Hamd meneja msaidiz, ndugu omar katibu mwenez na ndugu Tabu mohd mweka hazina na kujikuta ikishuka daraja na kucheza ligi daraja la kwanza kanda ikiwa imejikusanyia point 26 sawa na sawa na mabingwa wa zamani timu ya Mlandege ya visiwani Zanzibar. timu hiyo kwa sasa inaendeshwa na kaimu rais ndugu Ali Ramadhan (ndege) na kusaidiana viongozi wengine

ilitoka katika gazeti la mseto

simba taabani


Enyimba yaimaliza Simba

2008-03-24 09:50:11
By Mwandishi Wetu


Simba jana ilidhihirisha bado haijapata dawa ya kuifunga Enyimba ya Nigeria baada ya kuchakazwa 4-0 katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika uliofanyika mkatika uwanja wa Enyimba mjini Aba.

Matokeo hayo ni marudio ya mwaka 2004, ambapo Simba ilichakazwa 4-0 katika mechi ya mtoano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika baada ya timu hizo kushindwa kufungana katika mchezo wa kwanza uliochezwa mjini Mwanza.

Simba pia ilipata kuchapwa 3-0 mjini Aba mwaka 2003 wakati timu hizo zilipokutana kwenye mechi ya makundi, hata hivyo, Simba ilikuwa imeifunga Enyimba 2-1 katika mchezo mwingine wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.

Kwa matokeo hayo, Simba ina kazi ya ziada ya kushinda 5-0 ili kusonga mbele kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa baada ya wiki mbili.

Timu hiyo, hata hivyo, ilipokea na kipigo hicho na kibaya zaidi kwa muda mrefu ililazimika kucheza na watu 10 baada ya kutolewa kwa kiungo wake tegemeo, Henry Joseph katika dakika ya 37.

Katika mchezo huo, ambao mwamuzi William Agogo alionekana wazi kutoa maamuzi mengi ya kutatanisha na alimtoa Joseph kwa madai ya kumchezea vibaya mshambuliaji hatari wa Enyimba, Worku Stephen.

Katika mchezo huo, ulioanza saa 10 za jioni kwa saa za Nigeria (saa 12 kwa saa za Tanzania), wenyeji walionyesha hawakuwa na mzaha wakati walipoweza kupata bao la kuongoza katika dakika ya saba tu.

Worku aliweza kuzamisha bao hilo baada ya mabeki wa Simba kuzubaa kumzuia wakidhani alikuwa ameotea.

Bao hilo lilifanya Simba wacharuke na mshambuliaji wa Simba, Athumani Machupa alipoteza nafasi nzuri ya kusawazisha katika dakika ya 26.

Enyimba, hata hivyo, iliweza `kuzawadiwa` na Kipa wa Simba, Juma Kaseja katika dakika ya 36.

Kaseja alipiga mpira kwa nia ya kwenda kwa mmoja wachezaji wake na Worku aliweza kuwahi na kupiga shuti kali lililopita kushoto kwa Kipa Kaseja.

Hata hivyo, baada ya moja dakika tu, Simba ilipata pigo baada ya kutolewa kwa Henry.

Lilikuwa pigo kwa Simba na ikalazimika sasa kucheza kwa muda mwingi kwa kujihami na kuweza kutoa mwanya kwa Enyimba kuishambulia vikali.

Pamoja na mashambulizi huyo ya Enyimba na pia mwamuzi Agogo naye alionekana wazi kutoa maamuzi ya kusaidia Enyimba.

Mathalani alipuuzia kuumizwa kwa Emmanuel Gabriel, ambapo alitibiwa kwa muda mrefu nje ya uwanja.

Mwamuzi huyo baadae alitoa penati kwa Enyimba baada ya Nico Nyagawa kucheza rafu ndani ya eneo la hatari.

Worku aliweza kuzamisha penati hiyo katika dakika ya 76 baada ya kupiga shuti kali lililopita kulia kwa Kaseja.

Baada ya hapo Simba ilionekana wazi kukata tamaa na Enyimba ikamalizia mauaji yake baada ya kupata penati nyingine katika dakika ya 88 iliyofungwa na Kali Uche.

Simba iliwakilishwa na:Juma Kaseja, Nicodemus Nyagawa, Nurdin Bakari, Kelvin Yondani, Henry Joseph, Mohamed Banka, Mussa Hassan `Mgosi`, Mohamed Kijuso (Juma Nyosso), Athumani Machupa (Joseph Kaniki), Emmanuel Gabriel na Ulimboka Mwakingwe.


SOURCE: Nipashe

historia ya kombe la afrika


Kombe la mataifa ya Afrika na Historia yake…
KOMBE la Mataifa ya Afrika (CAN), ndiyo michuano mikubwa ya soka katika bara la Afrika inayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Kwa mara ya kwanza, michuano hii ilifanyika mwaka 1957 na kuanzia mwaka 1968 ndipo utaratibu wa kuchezwa kila baada ya miaka miwili ulipoanza.
Katika mashindano ya kwanza mwaka 1957 timu shiriki zilikuwa kutoka mataifa matatu tu yaani, Misri, Sudan na Ethiopia.
Nchi nyingine ambayo ilitajwa kushiriki katika mashindano haya ni Afrika Kusini ambayo hata hivyo ilinyimwa nafasi hiyo kutokana na sera zake za ubaguzi wa rangi kwa wakati huo.
Baada ya hapo mashindano yameendelea kukua na kuzihusisha nchi nyingi zaidi na hivyo kuwezesha kuwapo kwa utaratibu wa mashindano ya awali ya kusaka tiketi ya kushiriki fainali zenyewe na hatimaye timu shiriki kufikia 16.
Historia ya Kombe la Mataifa ya Afrika inaanzia Juni mwaka 1956 katika mkutano wa tatu wa FIFA mjini Lisbon, Ureno, baada ya kiubuka wazo la kuanzishwa kwa CAF.
Hapo jambo kubwa lililofikiriwa ni kuanzishwa kwa mashindano ya Bara la Afrika ambayo yalifanyika kwa mara ya kwanza, Februari 1957 katika jiji la Khartoum, Sudan.
Katika mashindano haya hakukuwa na mechi za kufuzu ambako nchi nne waanzilishi wa CAF, Misri, Sudan, Ethiopia na Afrika Kusini zilipanga mahali pa kufanyika michuano hiyo.
Afrika Kusini ilifutwa katika michuano hiyo baada ya kukataa kutuma kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji weusi na wazungu weupe hali ambayo ilitosha kuifanya Ethiopia iende moja kwa moja hadi hatua ya fainali.
Hali hiyo ilisababisha pia kuchezwa mechi mbili tu hadi bingwa kupatikana, Misri iliumana na Sudan katika hatua ya Nusu Fainali na kushinda na baadaye kuifunga Ethiopia katika hatua ya fainali na kutawazwa bingwa wa kwanza wa CAN.
Ethiopia ilikuwa icheze Nusu fainali na Afrika Kusini ambayo iliondolewa na hivyo kubahatika kwenda fainali moja kwa moja.
Miaka miwili baadaye, Misri ilikuwa mwenyeji wa mashindano hayo yaliyofanyika katika jiji la Cairo, ambayo pia yalizishirikisha timu zile zile tatu na Misri ikatwaa ubingwa kwa mara ya pili kwa kuibwaga Sudan.
Mashindano yalizidi kupata umaarufu, mwaka 1962 yalifanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia na kwa mara ya kwanza kulikuwa na michuano ya awali ya kufuzu kushiriki fainali hizo ili kupata timu nne zitakazoshiriki hatua ya fainali.
Wenyeji Ethiopia na mabingwa watetezi Misri walifuzu moja kwa moja na timu nyingine mbili zilizoshiriki ni pamoja na Nigeria na Tunisia.
Kwa mara ya tatu, Misri ilifikia hatua ya fainali lakini safari hii iliangushwa na Ethiopia ambayo ilitwaa taji hilo baada ya kuibwaga, Tunisia katika hatua ya Nusu Fainali na baadaye kuiangusha Misri katika dakika za nyongeza.
Ghana ambao ni wenyeji wa fainali za CAN hapo mwakani, ilishiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1963 ikiwa mwenyeji na kulibeba taji baada ya kuibwaga Sudan, katika hatua ya fainali.
Miaka miwili baadaye, Ghana tena ililibeba taji hilo nchini Tunisia ikiwa na kikosi ambacho kilijaa wachezaji wapya huku waliotwaa taji hilo mwaka 1963 wakiwa wawili tu. Hadi hapo Ghana ilijiwekea rekodi ya kutwaa taji hilo mara mbili sawa na Misri.
Utaratibu wa fainali za mwaka 1968 ulibadilika kwa kujumuisha timu nane kati ya 22 zilizoshiriki katika hatua ya awali ya kuwania kufuzu, timu ambazo baadaye zilifuzu nane na kupangwa katika makundi mawili ya A na B.
Katika utaratibu huo mpya, timu mbili zilizofanya vizuri katika kila kundi zilisonga mbele katika hatua ya Nusu Fainali, mfumo ambao uliendelea kutumika hadi mwaka 1992.
Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) ilitwaa taji hilo kwa mara ya kwanza mwaka 1968 kwa kuifunga Ghana katika mechi ya fainali.
Katika fainali za mwaka 1968, mshambuliaji nyota wa Ivory Coast, Laurent Pokou aliibuka mfungaji bora akiwa amefunga mabao sita na kufanya hivyo tena katika fainali za mwaka 1970 kwa kufunga mabao manane.
Rekodi yake ya mabao 14 katika fainali mbili imeendelea kuwa rekodi ya kipekee katika michuano hiyo.
Fainali za mwaka 1970 zilifanyika nchini Sudan na kwa mara ya kwanza katika historia, fainali hizo zilianza kuonyeshwa kwenye Televisheni huku wenyeji wakibeba kombe hilo baada ya kuwabwaga Ghana ambao walikuwa wakifikia hatua hiyo kwa mara ya nne mfululizo.
Kuanzia mwaka 1970 hadi 1980 nchi sita zilitamba katika michuano hiyo kwa kuibuka vinara, nchi hizo ni Sudan, Congo Brazaville waliolibeba mwaka 1972, Zaire (DRC) Morocco, Ghana na Nigeria.
Zaire ilibeba kombe hilo kwa mara ya pili mwaka 1974 (awali ililitwaa ikiwa inatumia jina la DRC kabla ya kubadili na kuwa Zaire na sasa kurudia jina la DRC) baada ya kuilaza, Zambia katika mechi ya fainali.
Mechi hiyo ya fainali ililazimika kuchezwa mara mbili baada ya timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2 katika dakika za nyongeza na kurudiwa siku mbili zilizofuata ambako Zaire ilishinda kwa mabao 2-0.
Katika mechi hizo, mabao yote manne ya Zaire katika mechi hizo mbili yalifungwa na mshambuliaji wao, Mulamba.
Morocco kwa mara ya kwanza ilibeba taji hilo mwaka 1976 nchini Ethiopia wakati Ghana ililibeba taji kwa mara ya tatu mwaka 1978 na kuwa nchi ya kwanza kujiwekea rekodi ya kubeba taji hilo mara tatu.
Mwaka 1980, Nigeria ilikuwa mwenyeji wa fainali hizo ambazo pia Tanzania ilishiriki na wenyeji Nigeria walifanikiwa kulibakisha kombe nyumbani baada ya kuilaza, Algeria katika fainali.
Ghana iliendeleza ubabe mwaka 1982 kwa kulitwaa kombe nchini Libya, ilianza kwa kuinyuka, Algeria katika hatua ya Nusu Fainali na kuumana na wenyeji Libya katika mechi ya fainali kwa mikwaju ya penalti.
Miaka miwili baadaye, Cameroon walibeba taji hilo kwa kuilaza Nigeria na mwaka 1986 walifikia hatua ya fainali na kuumana na Misri lakini ni Misri ndio walioibuka vinara kwa mikwaju ya penalti.
Mwaka 1988, nyota ya Cameroon iling’ara baada ya kufikia hatua ya fainali na kulibeba kombe kwa ushindi dhidi ya Nigeria wakati mwaka 1990, Nigeria ilianguka tena na kujikuta ikishindwa kulibeba kombe ambalo lilichukuliwa na Algeria.
Katika fainali za mwaka 1992, idadi ya timu iliongezeka na kufikia 12 ambazo ziligawanywa katika makundi manne, kila kundi lilitoa timu mbili zilizosonga mbele katika hatua ya Robo Fainali.
Mchezaji mahiri wa Ghana, Abedi Pele Ayew ambaye alifunga mabao matatu katika fainali hizo ndiye aliyetangazwa kuwa mwanasoka bora wa fainali hizo kutokana na mchango wake ulioiwezesha timu hiyo kufikia hatua ya fainali.
Hata hivyo, katika mechi ya fainali dhidi ya Ivory Coast alitolewa nje na timu yake ilishindwa kufurukuta.
Utaratibu wa timu 12 uliendelea mwaka 1994 nchini Tunisia ambako wenyeji walijikuta wakilala katika hatua ya kwanza na Nigeria ambao ndio waliofikia fainali na kuibwaga Zambia hadi kutwaa taji.
Nigeria ambayo wakati huo ilifuzu kwa mara ya kwanza fainali za Kombe la Dunia iliwafunga Zambia ambao mwaka mmoja kabla ya fainali hizo ilipatwa na msiba mkubwa wa kufiwa na nyota wake waliokufa katika ajali ya ndege. Rashid Yekini, mshambuliaji wa Nigeria aliibuka kinara wa upachikaji mabao akiwa na mabao matano, Yekini katika fainali za mwaka 1992 aling’ara kwa mabao manne.
Mwaka 1996, Afrika Kusini ilikuwa mwenyeji ikishiriki kwa mara ya kwanza baada ya kusimamishwa kutokana na sera za ubaguzi wa rangi zilizokuwa zikitawala nchini humo.
Timu ziliongezwa na kufikia 16 ambazo ziligawanywa katika makundi manne ingawa baadaye timu hizo zilibakia 15 baada ya Nigeria kujitoa katika hatua za mwisho kwa sababu zilizotajwa kuwa ni za kiusalama.
Afrika Kusini ikiwa na kikosi maarufu cha Bafana Bafana ililibakisha taji hilo nyumbani na nahodha wa timu hiyo, Neil Tovey akawa mzungu wa kwanza kulibeba juu kombe hilo.
Miaka miwili baadaye fainali hizo zilipigwa nchini Burkina Faso ambako Afrika Kusini ilifurukuta na kukawa na matumaini makubwa ya kulibeba taji hilo lakini timu hiyo ilishindwa kutamba mbele ya Misri walioibuka vinara.
Mwaka 2000 fainali ziliandaliwa kwa ushirikiano wa nchi za Ghana na Nigeria ambao walichukua nafasi ya Zimbabwe iliyoandaliwa kuwa mwenyeji.
Cameroon ilifanikiwa kulibeba taji hilo baada ya kuibwaga Nigeria kwa mikwaju ya penalti. Mambo yaliinyookea tena Cameroon au Indomitable Lions mwaka 2002 kwa kuwafunga Senegal ambao walifikia hatua ya fainali kwa mara ya kwanza na mwaka 2004 wenyeji Tunisia walifanikiwa kulibakisha kombe nyumbani baada ya kuilaza, Morocco kwa mabao 2-1.
Mwaka 2006, kombe pia lilichukuliwa na wenyeji, Misri, ambao pia walijiwekea rekodi ya kubeba taji hilo kwa mara ya tano, Misri wakiwa nyumbani mjini Cairo waliibwaga Ivory Coast katika fainali.
Bila shaka kwa sasa anasubiriwa kwa hamu kinara wa taji hilo kwa mwaka 2008.
Rekodi za washindi wa CAN tangu kuanzishwa kwake…
Mwaka Nchi iliyoshinda
1957 Misri
1959 Misri
1962 Ethiopia
1963 Ghana
1965 Ghana
1968 DRC
1970 Sudan
1972 Congo Brazzaville
1974 DRC
1976 Morocco
1978 Ghana
1980 Nigeria
1982 Ghana
1984 Cameroon
1986 Misri
1988 Cameroon
1990 Algeria
1992 Ivory Coast
1994 Nigeria
1996 Afrika Kusini
1998 Misri
2000 Cameroon
2002 Cameroon
2004 Tunisia
2006 Misri
2008 Misri